Kama sio DStv potezea
TECNO Spark 2

Michezo

Video:SportPesa wameniongezea elimu – Okwi

By  | 

Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Uganda na klabu ya Simba, Emmanuel Arnold Okwi amesema ziara yao ya kwenda katika kampuni ya kubashiri matokeo ya SportPesa ambao ndiyo wa dhamani wao wa kuu imemuongezea elimu ya namna ya kujitambua na kujiongezea thamani kama mchezaji.

Okwi ambaye ni miongoni mwa wachezaji waliyosajili msimu huu na klabu ya Simba ameyasema hayo kupitia mahojiano na Bongo5.

“ Tumepata nafasi kubwa sana na muhimu ya  kuwatembelea wadhamini wetu wa kuu na nafikiri ni changamoto kwetu kama wachezaji kwa kuwa wametuambia mambo mengi sana ambayo tulikuwa hatuyajui sasa tumeweza kuyajua na tunayafanyia kazi.”Amesema Okwi.

Emmanuel Okwi ameongeza “Kunamambo ya kuyafanyia kazi sisi kama wachezaji ili tuweze kufaidika na SportPesa kwakweli ni chansi kubwa sana kuwa hapa tunajiskia furaha.”

“Nilikuwa najitahidi sana kujiweka mwenye thamani lakini kwa leo nimepata elimu zaidi na nafikiri nikitua ambacho nitakifanyia kazi zaidi nilichokipata hapa.”

Wachezaji wa timu ya Simba na baadhi ya viongozi wake wamepata bahati ya kutembelea Ofisi za kampuni ya kubashiri matokeo ya SportPesa ambao hudhamini klabu za Simba SC,Yanga SC na Singida United zote zikiwa zinashiriki ligi kuu ya Tanzania Bara.

Loading...

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Comments

Bongo5

FREE
VIEW