Habari

Video:Taarifa ya fedha za posho za walimu nchini

By  | 

Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi, Utumishi na Utawala Bora, Seleman Jafo Selemani amesema serikali kuanzia mwezi Julai 2016 hadi 2017 Serikali imelipa walimu jumla ya shilingi Bilioni 1.87 kwa ajili ya kuimarisha usimamizi wa elimu katika ngazi za shule nchini.

Naibu Jafo, amezungumza hayo Bungeni leo mjini, wakati akijibu swali la Mbunge wa Mafinga Mjini, Mhe Cosato Chumi lililouliza Je,

Ni lini serikali itaanza kulipa posho hiyo ya viongozi wa elimu?

“Serikali ilianza kutekeleza sheria namba 3 ya mwaka 2014, kuhusu posho ya madaraka kwa viongozi kuanzia mwezi Julai 2016 walimu wakuu wanalipwa kiasi cha fedha laki 2 kwa mwezi, na wakuu wa shule na waratibu wa Elimu kata wanalipwa posho ya madaraka kwa kiwango cha shilingi laki 2 na nusu kwa mwezi,” alisema Jafo.

“Kuanzia mwezi Julai 2016 hadi 2017 Serikali imelipa posho hiyo jumla ya shilingi Bilioni 1.87 posho hiyo inalipwa kwa viongozi hao kwaajili ya kuimarisha usimamizi wa Elimu katika ngazi za shule nchini.”

Video: Naibu Waziri Seleman Jafo anatoa majibu ya Serikali

Na Emmy Mwaipopo

Loading...

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Comments