Habari

Vifahamu viambato vilivyopigwa marufuku kutumika kutengeneza vipodozi

Kila mtu alimtazama na alimzungumzia kila alipopita, Lahasha! Namzungumzia Mariam binti wa miaka 20, mwanafunzi wa wa mwaka wa 3 katika chuo kikuu cha Dar es Salaam. Alikuwa na weupe wa kung’aa kiasi kwamba usingeweza kutambua kuwa ni mwarabu, muasia, au muhindi.

Kila alipopita hadi wasichana wenzake walimtamani, maskini hawakujua siri ya urembo wake. Ama hakika jambo usilolijua ni sawa na usiku wa giza. Muda huu tunapoongea, ukitazama picha yake ya miaka miwili nyuma ni tofauti na muonekano wake wa sasa. Ukimfananisha na bibi wa miaka 65 ungezani Mariam ni mkubwa zaidi yake.

Vipodozi vimemfanya avutie kwa muda mchache na achukize kwa mda mrefu. Tambua viambato ambavyo vimepigwa marufuku kutumika kwenye kutengeneza vipodozi.

Viambato vyenye sumu vilivyopigwa marufuku;-

1.Bithionol
2.Hexachlorophene
3.Mercury compounds (zebaki)
4.vinyl chloride
5.Zirconium-containing complexes in aerosol products
6.Halogenated salicylanilides (di-,tri-metabromsaln and tetrachlorosalicynilide)
7.Chloroquinone and its derivatives
8.Steroids in any proportional
9.Chloroform
10.Chlofluorocarbon propellants
11.Methylene chloride
12.Hydroquinone
13.steroids
14.Tin oxide

Viambato hivi hupatikana kwenye krimu, losheni, jeli ,sabuni za maji ya kujipaka, sabuni, vipodozi vya vya kuzuia harufu (Antiperspirants), vipodozi vya kupunguza unene vyenye viambato vyenye mmea (Phytolacea spp). Pia kuna baadhi ya mimea ambayo imethibitika kua na viambato hatari kutumika kwenye vipodozi

Kama vile ;-
1.Arctostaphylos UVA URSI (bearberry extract)
2.Apocynum Cnnabium root extract
3.Tussilago farfara

Na vipodozi vingine vyenye viambato vya dawa za tiba na matumizi mabaya ya dawa kama vipodozi kama ifuatavyo;-

1.Moja kati ya viambato vilivyopigwa marufuku kutumika kama kipodozi ni ‘steroids’ ambazo kimsingi ni dawa. Mfano wa viambato hivi ni pamoja na clobetasol na betamethasone zinazopatikana kwenye dawa aina ya Movate, Betacort-N, Diproson, Gentrisone n.k

2.Bidha hizo apo juu ni lazima kutumika kama dawa za cheti (prescription only medicines) na lazima kutolewa kwa wagonjwa wa ngozi kwa kufuata maelezo ya daktari na mfamasia na hazirusiwi kutumika kama vipodozi.

3.Pia ni hatari kutumia dawa zenye viambato hivi kwa minajidi ya kuongeza makalio na maziwa.

YAFUATAYO NI MADHARA YATOKANAYO NA MATUMIZI YA VIPODOZI VYENYE VIAMBATO VYENYE SUMU

i.Biothinol-kupata mzio wa ngozi na athari kwenye ngozi ikiwa itapata mwanga wa jua.

ii.zebaki(Mercury)-husababisha madhara ya ngozi, ubongo,figo na viungo mbalimbali vya mwili, Zebaki inapopakwa kwenye ngozi huweza kupenya ndani ya mwili na kusababisha sumu yake kuingia kwenye damu na kusababisha madhara mengi. ‘mama mjamzito akitumia vipodozi vyenye zebaki motto huathirika akiwa bado tumboni na huzaliwa akiwa na mtindio wa ubongo”|.
Pia husababisha mzio wa ngozi na muwasho

iii.Zirconium –husababisha kansa ya ngozi na mapafu

iv.Halogenated salicylanilide- husababisha mzio wa ngozi mara inapopata mwanga wa jua na pia husababisha ugonjwa wa ngozi

v.Hydroquinone-Husababisha muwasho wa ngozi, mzio wa ngozi, saratani, kuchubuka kwa ngozi na kusababisha mabaka meupe.

vi.Steroids-steroids ni kundi la homoni. Homoni hizi hutengenezwa na mwili wa binadamu. Lakini pia zinaweza kutengenezwa nje ya mwili wa binadamu (artificial hormones). Katika kundi hili, corticosteroids ndizo ambazo hutumikla sana. Steroids zikitumika kwa muda mrefu husababisha madhara mbalimbali kama;ugonjwa wa ngozi na kutokwa na chunusi kubwa. Pia ngozi huwa nyembamba na laini na endapo itapata jeraha au kufanyiwa upasuaji, kidonda hakitapona. Pia husababisha magonjwa ya moyo.

vii.Chloroform-husababisha kansa ya utumbo mpana na kibofu cha mkojo,pia husababisha ugonjwa wa akili na ugonjwa wa mishipa ya fahamu, kwenye ngozi, chloroform husababisha ngozi kuungua, maumivu makali, ngozi kuwa nyekundu sana na kutokwa vipele.

WITO WANGU NI KWAMBA, NAFAHAMU UREMBO NI JAMBO LISILOZUIRIKA KWA DADA ZETU LAKINI NI VEMA KABLA YA KUNUNUA KIPODOZI SOMA KWANZA KAMA HAINA VIAMBATO NILIVOVIAINISHA HAPO JUU NDIPO UNUNUE. IJALI AFYA YAKO KWANZA

YOUR HEALTH, MY CONCERN

BY FORD A. CHISANZA
Intern pharmacist
Tanzania Food And Drug Authority (TFDA)
Location: Off Mandela Road, Mabibo – External,
P.o.Box: 77150, Dar Es Salaam, Tanzania.
Mobile:+255 652466430/+255 684363584
Email: [email protected]

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents