Burudani

Vigezo saba vya kulinasa penzi la Lulu Diva

Msanii wa Bongo Flava, Lulu Diva ametaja vigezo saba ambavyo mwanaume yeyote akiwa navyo basi yupo tayari kuingia nae katika mahusiano.

Muimbaji huyo ameeleza kuwa licha ya vigezo hivyo, kwanza mwanaume huyo anapaswa kujua kwamba yeye ni msichana ambaye anapenda sana kudekezwa.

“Kwanza kabisa nampenda mwanaume smart mind, mtu ambaye ameshika dini anamuheshimu Mungu, pia gentlemen kama hivyo awe ananidekeza awe ananijali, listen, understanding, passion na Sacrifice,” ameiambia Mambo Mseto ya Citizen Radio.

Pia ameongeza kuwa licha ya kupenda kudekezwa, yeye ni msichana mtafutaji na mrembo, hivyo hababaishwi na vitu vidogo.

By Peter Akaro

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents