Habari

Vijana 100 wa DIT na vyuo vingine wapata ajira Saudia kupitia Bravo Agency

Kampuni ya Uwakala wa Ajira Nchini Tanzania, Bravo Job Agency ya mwanasiasa mkongwe nchini, Abbas Zuberi Mtemvu imefanya usahili Jumatano hii katika viwanja vya Taifa jijini Dar es salaam kwaajili wa kuwapata vijana zaidi ya 100 wenye taaluma mbalimbali wataokwenda kufanya kazi nchini Saudi Arabia kupitia kampuni kubwa ya nchini humo, Al-Marai.

Vijana wakisubiria usahili mapema leo.

Tukio hilo limekuja ikiwa ni wiki mbili toka kampuni hiyo iwasafirishe vijana zaidi ya ishirini wenye taaluma mbalimbali kwenda nchini humo huku wengi wakionyesha kufurahishwa na hatua ya kampuni hiyo ya kuwatafutia ajira.

Akiongea na waandishi wa habari Jumatano hii, Mkurugenzi wa Kampuni hiyo, Abbas Mtemvu akiwa katika usahili huo nyuma ya uwanja wa Taifa, amesema mpaka sasa wamejitokeza vijana wengi katika usaili huo huku akidai kuna vijana wa vyuo mbalimbali vikuu nchini Tanzania, wakiweno vijana kutoka chuo cha Dar Es Salaam Institute Of Technology (DIT).

“Vijana wameanza kuona mambo mazuri na kweli namamiminika kwenye usahili, ukiachana na madereva wa magari makubwa na madogo ambao wamekuwa wakijitokeza kwa wingi sasa hivi baada ya kutangaza ajira nyingi zaidi pamoja na za watu wa IT, Mechanical engineer, mafungi mafriji pamoja na AC, Sales, kusema kweli mambo ni mazuri zaidi na kwasasa kuna vijana zaidi ya 100 wamepatikana na tunaendelea kufanya usaili kwa sababu tumepata nafasi nyingi zaidi,” alisema Abbas.

Mkurugenzi wa Bravo Job Agency, Abbas Mtemvu.

“Tunaomba watanzania wajitokeze zaidi kwa sababu bado tunazo nafasi 2000 sales Man, na assistant sales man,wapishi, Mainjinia,Madereva wa Magari Makubwa,Mainjinia wa Refregration and air Condition,machenical,na oparetor wa Plastic Mashine kwa hiyo niwaambie tu watanzania kwamba Bravo inamuunga mkono Mh Rais Magufuli kuhakikisha watanzania wanapata ajira, na Al-marai ni Kampuni kubwa sana inayotambulika kiserikali,” aliongeza Mtemvu.

Pia Mtevu alimshukuru Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia, Balozi Mgaza pamoja na team yake kwa kuwakikisha watanzania wanapata fursa za ajira ambazo zinamaslahi na tija kwao.

“Serikali ya Magufuli ni ya kazi, ndio maana unasikia Hapa Kazi Tu, kila mtu anatakiwa kufanya kazi, sisi Bravo kwa kushirikiana na ubalozi wa Saudia tumeona kuna fursa kubwa sana Saudia ndio maana tumeona tuwanufaishe watanzania kwa kupata kazi bora ambazo zina mishahara minono, nyumba za kulala wafanyakazi ni mzuri, yaani maisha ni mazuri,” alisema Abbas Mtemvu.

Kwa Upande wake Iddi Mawad ambae amepita katika usahili huo amewataka wananchi kujitokeza kufanya usahili nakusema kuwa katika kampuni hiyo hakuna udanganyifu wowote kama taarifa zuilizoenea mitaani.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents