Michezo

Vijana 5 wakidhi vigezo vya kushiriki Mashindano ya Dunia

Mashindano ya Kanda ya tano maarufu kwa jina la “EASTERN AFRICAN ATHLETIC REGION (EAAR)” yamemalizika hapo jana ambapo yameshirikisha jumla ya nchi 7 huku Tanzania akiwa mwenyeji wa mashindano hayo kwa mwaka huu.

Mashindano hayo yalishirikisha michezo mbalimbali ikiwemo Mbio fupi, Miruko pamoja na Kurusha Mitupo, yaliyoanza kutimua vumbi May 13 hadi 14 mwaka huu, yalifanyika katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam huku Tanzania ikifanikiwa kutoka kimaso maso kwa kuchomoza na Medali nyingi zaidi ukilinganisha na nchi nyingine zilizoshiriki.

Hata hivyo Kenya imeshika nafasi ya kwanza  katika mashindano hayo kutokana na kujinyakulia Medali nyingi zaidi za dhahabu. Kenya imekusanya jumla ya Medali za dhahabu 8 na kuiacha Tanzania ikivuna Medali za dhahabu 7 ikiizidi za dhahabu 1, kwa jumla ya Medali zote Tanzania imelingana na Kenya na hivyo kushika nafasi ya pili katika mashindano hayo ukilinganisha na mashindano ya mwaka jana ambayo Tanzania ilishika nafasi ya 4.

Pamoja na Medali hizo, Tanzania imefanikiwa kupata vijana watano ambao wametimiza vigezo vya kushiriki mashindano ya Dunia ambayo yanatarajiwa kufanyika Nairobi mwezi wa 7.
BY HAMZA FUMO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents