Habari

Vijana kuna kazi azihitaji uzoefu, unaweza ukagombea Udiwani na Ubunge – Spika Ndugai

Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai amewataka vijana nchini kugombea nafasi ambazo hazihitaji uzoefu kama udiwani na Ubunge.

Spika Ndugai amesema hayo Bungeni leo, Mei 18, baada majibu ya Mbunge wa viti maalumu Zainab Katimba aliyetaka mkakati wa Serikali katika kutatua tatizo la ajira kwa vijana wasomi wasio na uzoefu(Work Experience).

“Asante sana Waziri wa nchi kwa majibu ya nyongeza, eeh vijana wasomi, zipo kazi nyingine hazihitaji uzoefu, mnagombea Udiwani, mkagombea Ubunge, nawatangazia vita waheshimiwa hapa,” Spika Ndugai alitoa kauli hiyo akicheka.

Aidha serikali kupitia Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Vijana na Watu Wenye Ulemavu, Anthony Mavunde imesema imetafuta ufumbuzi wa tatizo la uzoefu wa ajira kwa kushirikiana na Waajiri, vyama vya wafanya kazi kwa kutafuta Makampuni mbalimbali ili vijana waende kusoma na kujipatia vyetu vya uzoefu ili kuepuka usumbufu wakati wa kutafuta ajira.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents