Michezo

Vilabu vya Tanzania vimeshindwa kuendeleza wachezaji wazawa

Mcheza kwao hutunzwa, lakini hili limekuwa tofauti kwa wachezaji wa Tanzania hasa wanaocheza ligi kuu ya Vodacom.

P 21

Nilihuzunika sana lakini pia nilivutiwa na kauli ya Samatta aliposema, “Niligoma kuichezea Simba kwa muda kwasababu timu hiyo walishindwa kunipatia gari kama tulivyokubaliana japo hili halikuwa ndani ya mkataba wetu.” Je kuna wachezaji wangapi ambao timu zao zinavunja masharti yao makusudi na kuwanyonya wachezaji hao ambao ni hazina kwa taifa. Je unakumbuka kilichomtokea Oscar Joshua na Yanga? Unakumbuka Joseph Owino na Simba?

Sheria za TFF zinasema kila timu inayoshiriki ligi kuu inatakiwa iwe na timu ya vijana kwaajili ya kuinua soka la nchi. Sina uhakika kwenye hili kama limetekelezwa kwa asilimia 100, ila nachojua kuwa yakikaribia mashindano ya Uhai Cup baadhi ya timu zinaanza kuingia mtaani na kuokoteza vijana ili washiriki michuano hiyo.

Wako wapi wachezaji kama Kigi Makasi, Amir Maftah, Jerryson Tegete, Edward Christopher, Sitaki kumkumbuka Uhuru Selemani wa Shabani Kado. Hawa ndio walionekana kuja kuwa kama kina Walcot, Charmberlin, Sterling leo hii pale Uingereza au Paul Pogba na Antonio Grienzman pale Ufaransa. Nikiiangalia La Masia napata picha nyingine kabisa na kuwaona wakina Messi wengine wakizidi kuzaliwa kuchukua nafasi ya huyu wa leo muda utakapomtupa mkono.

mbwana-samatta_2nx5mzohoms410k2eiy1i42zn

Shukrani kwa Mbwana Samatta ameweza kujituma hadi kufikia hatua ya kuweka historia kuwa mchezaji wa kwanza Afrika Mashariki kuchukua tuzo ya mchezaji bora wa Afrika kwa wachezaji wanaocheza Afrika. Kwa hili lililotokea kwa Samatta siyo Simba walioibua kipaji cha mchezaji huyu, asilimia kubwa ni uwezo wake wa kujituma, nidhamu na kutokata tamaa ndio kumemfikisha hapa leo.

ngasaaaaa

Tanzania ni miongoni mwa nchi zenye wachezaji wenye vipaji kama Brazil, lakini ubabaishaji wa viongozi wa vilabu wanaowachukua wachezaji hao na kuanza kuzizima ndoto zao kidogo kidogo. Nilitegemea leo hii nikimuona Ngassa kwenye TV akicheza Ulaya akipambana na mabeki kama John Terry, Vincent Kompany, Gerard Pique, Giorgio Chiellini na wengine kibao.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents