Michezo

Vilabu vya Uingereza vyaongoza kwa kutumia gharama kubwa kwenye usajili, vyatumia kiasi hiki

Vilabu vya Uingereza vyaongoza kwa kutumia gharama kubwa kwenye usajili, vyatumia kiasi hiki

Usajili wa wachezaji dakika za mwisho ulivifanya vilabu vya Ligi ya PremiA kutumia hadi £1.41bn, karibu kufikia rekodi ya £1.43bn iliyowekwa 2017, kwamujibu wa kampuni ya uhasibu ya Deloitte. bFedha zilizotumiwa na vilabu vikubwa siku ya mwisho ya uhamisho wa wachezaji ilikua £170m -kukamilisha mikataba 17 pekee, ikilinganishwa na idadi ya uhamisho wa siku ya mwisho kutoka tangu 2009.

Hatua ya Everton ya kumsajili kwa £34m mshambuliaji Alex Iwobi kutoka Arsenal imetajwa kuwa mkubwa, huku uhamisho huo pia ukimsaidia Romelu Lukakukuondoka kwenda kwa kima cha £74m – hasara ya £1m ya ada waliolipaEverton. Arsenal walitumia jumla ya £155mkuwanunua wachezaji kabla ya dirisha la usajili kufungwa.

Siku ya mwisho ya ya shughuli hiyo ilitumia £25m kumnunua beki wa kushoto wa Celtic Kieran Tierney na £8m kumnyakua beki wa ka Chelsea David Luiz. Tottenham ilimsajili kwa mkopo kiungo wa kati wa Real Betis Giovani lo Celsopamoja na winga Fulham Ryan Sessegnon kwa £25m.

Kwa mujibu wa BBC. Watford ilivunja rekodi ya matumizi yake inayoripotiwa kuwa £25m, kumnunua winga Ismaila Sarr nayo Leicester ikajipatia mshambuliaji wa kati wa Sampdoria Dennis Praet kwa £18m. Wachezaji watatu wa zamani wa kimataifa walihama – Burnley ilimsajili kingo wa kati wa Chelsea Danny Drinkwater na Manchester City wakamchukua kipa wa Derby Scott Carson, wote kwa mkopo, huku Newcastle wakimsajili tena mshambuliaji Andy Carroll .bila malipo.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents