Habari

Vimwana wa Twanga Pepeta wajipanga kwa fainali

manywele_mpya_face 

(Baadhi ya washiriki walioingia kumi bora katika shindano la Kimwana wa Twanga Pepeta 2011, kutoka kushoto ni Johari Juma, Amanda Cyprian, Rehema Said, Mariam Mwakyoma na Amina Juma.)  Washiriki wa Shindano la Kimwana wa Twanga Pepeta 2011 wameiva

 


na wako tayari kwa ajili ya Fainali za Kimwana wa Twanga Pepeta 2011 zinazotarajiwa kufanyika katika ukumbi wa Ubungo Plaza Ijumaa tarehe 08-07-2011.

Vimwana hao ambao wameongezewa Mwalimu wa kuwafundisha kucheza ili waweze kufanya vizuri katika Fainali za Shindano hilo. Hapo awali walikuwa wakifundishwa na Kassim Mohammed au “Super K” lakini kwa sasa wameongezewa mwalimu atakayesaidiana naye ambaye ni Bakari Kisongo aka “Mandela”.

Manyweleo_mpya

( Baadhi ya washiriki walioingia kumi bora katika shindano la Kimwana wa Twanga Pepeta 2011, kutoka kushoto ni Hawa Miraji, Salha George, Leila Mshana, Mary Hamis na Edina Amani.)

Washiriki walioingia Kumi Bora kama wanavyoonekana kwenye picha ni pamoja na Leila Mshana, Mary Hamis, Mariam Mwakyoma, Amina Juma, Hawa Miraji, Amanda Cyprian, Rehema Said, Johari Juma, Edina Amani na Salha George.

Mshindi atakayeibuka Mshindi atajinyakulia zawadi ya Duka la Vipodozi lililogharimu kiasi chaa shilingi milioni tano ambalo lishapatikana lipo Kinondoni Studio jirani na kituo cha Daladala.

 



Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents