Habari

Viongozi 18 wajiengua ACT Wazalendo, Polepole adai CCM itatawala milele

Zoezi la kuhama hama vyama bado linaendelea ambapo leo viongozi 18 wa chama cha ACT Wazalendo kutoka mikoa mbalimbali nchini wamejivua nyadhifa zao na kujiunga na CCM.

Humphrey Polepole

Zoezi hilo la kuwapokea Wanachama hao wapya limefanyikaa leo Januari 17, 2018 mjini Moshi na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira ambaye hata yeye alishawahi kuwa mwenyekiti wa ACT kabla ya kujiunga na CCM..

Akitoa hotuba fupi baada ya kupokea wanachama hao, Polepole amesema katika kipindi cha miaka miwili ya utawala wa Serikali ya Awamu ya Tano, CCM imeongeza wanachama zaidi ya milioni mbili na kwa mwendo huo basi chama hicho huenda kikatawala nchi milele.

Tukisimamia haki na heshima kwa watu wote CCM itatawala milele nchi hii. Kwa sababu misingi ya chama hiki ni utu. Sasa tunahitaji watu ambao wanachukizwa na rushwa, ubadhirifu na ubinafsi,”amesema Polepole.

Miongoni mwa wanachama hao, wapo waliokuwa wajumbe wa kamati kuu, wenyeviti wa mikoa na makatibu wa ACT Wazalendo.

Wakieleza sababu za kukihama Chama cha ACT Wazalendo wengi wamesema wamechukua maamuzi hayo kutokana na sababu mbalimbali, ikiwemo ya viongozi waandamizi wa chama hicho akiwemo RC Mghwira  kuhamia CCM.

Baadhi ya majina ya viongozi  wa ACT Wazalendo waliohama ni Eva Kaka (mjumbe  Kamati Kuu),  mwenyekiti wa Mkoa wa Dodoma Anganile Massawe, Athuman Balozi (mwenyekiti mkoa wa Tabora), Hamad Nkya (mwenyekiti mkoa wa Kilimanjaro), Godwin Kayoka (katibu wa mkoa Tabora) na Juma Hamisi (mwenyekiti wazee mkoa wa Singida).

Chanzo:Mwananchi

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents