Viongozi wa dini msiwe na wasemaji ambao sio viongozi – Rais Magufuli (+video)

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amewaomba viongozi wa dini zote kutokuwa na wasemaji ambao si viongozi wa dini.

Rais Magufuli ameyasema hayo leo, Juni 12, 2018 alipotembelea kukagua msikiti mkuu wa Baraza Kuu la Waislam(BAKWATA) unaojengwa eneo la Kinondoni Jijini Dar es Salaam ambapoa amesema kuwa wakiwatumia viongozi wa siasa watakuwa wanachanganya dini na siasa.

“Napenda kuwaahidi viongozi wa dini zote kwamba serikali yangu itaendelea kushirikiana na dini zote na niendelee kuwaomba viongozi wa dini, msiwe na wasemaje ambao sio viongozi wa dini mnapokuwa viongozi wa dini alafu mkawatumia wasemaji ambao si viongozi wa dini labda wanasiasa mtakuwa machanganya dini na siasa ambacho ni kitu kibaya sawa kwahiyo panapozungumzwa suala lolote linalohusu mambo ya dini au ushauri wowote unaohusika na dini uzungumzwe na watu wa dini wenyewe,” amesema Rais Magufuli.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW