Habari

Viongozi wastaafu walitumika kama kichaka – Waziri Nchemba

Waziri wa Mambo ya Ndani, Mhe. Mwigulu Nchemba amempongeza Rais Magufuli kwa kulinda rasilimali za nchi huku akimpongeza kwa hatua aliyoifanya dhidi ya wanao wahusisha viongozi wastaafu katika ripoti ya Makinikia.


Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mwigulu Nchemba

Waziri Nchemba ameyazungumza hayo akiwa kwenye ziara Jimboni kwake Iramba Magharibi ambapo aliweka wazi kufurahishwa na Rais alipotaka viongozi hao Wastaafu waachwe wapumzike.

“Rais wetu amechukua hatua kwa vitendo, tumuunge mkono walivyoona vichaka vyote hivyo vimeisha wakaanza kutaja wakidhania hicho kitakuwa kitu cha kuzuia ili jitihada hizo zisiendelee, wakaanza kutaja viongozi waliostaafu ile yote si kwamba walikuwa wanataja viongozi wale kama walikuwa wametumika, walitumia kama kichaka kwamba unajua sasa tukiwataja wale unajua wataacha, ngoja niwaambie viongozi wetu hawa hawajawahi kuwa maajenti wa wale wanao tuibia, maajenti tumewaona wanao watetea na mimi nimpongeze sana Rais wetu akauona ule mtego akafyatua pyaa, sasa hivi kama ni gari lao Mheshimiwa Rais ameshaondoa upepo matairi yameshalala chini,”alisema Waziri Mwigulu.

“Sasa kwa maombi yenu na dua zenu kila mtego wakiweka anafyatuka tena unafyatuka, kabla mfyatuaji hata hajafika tuendelee kumuombea Rais wetu kwa kuhakikisha rasilimali za nchi yetu haziibiwi, ndizo zitakazo tuwezesha kupata maji, ndizo zitakazo tuwezesha kupata barabara,rami, umeme, elimu bure ndizo zitakazo tuwezesha tupate dawa,”

“Lakini kitu kingine kizuri alichokifanya Muheshimiwa Rais akatokea wazi kuwaambia wote wawaache wazee wetu wapumzike unajua heshima ya nchi yetu, heshima ya watu kuheshimu kazi walizofanya kazi nzuri viongozi wastaafu ni moja ya sifa inayofanya na taifa letu viongozi wasinga’nga’nie madarakani,” aliongeza Mwigulu.

Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents