Michezo

Viongozi wawili wa juu wa klabu ya Yanga wajiuzulu, wamtaja atakayeiongoza klabu hiyo kwa sasa

Viongozi wawili wa juu wa klabu ya Yanga ya Jijini Dar Es Salaam, wamejiuzulu nafasi zao, mapema leo Machi 27, 2019 mchana.

Viongozi hao waliojiuzulu ni aliyekuwa Kaimu Mwenyekiti wa klabu hiyo, Samwel Lukamay na aliyekuwa mjumbe wa kamati ya utendaji, akishikilia nyadhifa za Mwenyekiti wa Kamati ya mashindano na Mwenyekiti wa Kamati ya usajili, Hussein Nyika.

Lukumay na Nyika wametangaza maamuzi hayo, kwenye makao makuu ya klabu hiyo ambapo wamefanya hivyo ili kupisha uchaguzi mkuu utaowezesha klabu kupata viongozi wapya.

Ninajiuzulu nafasi zangu zote nikiwa kama Mjumbe wa kamati ya utendaji lakini pia Mwenyekiti wa kamati ya usajili na kamati ya mashindano na niombe msamaha kwa wale niliowakosea katika utekelezaji wangu wa majukumu’‘, amesema Nyika.

Kwa upande wake, Lukumay amesema Yanga kwa sasa inakabidhiwa kwa wanachama kupitia kwa Baraza la Wadhamini la klabu hiyo linaloongozwa na George Mkuchika.

Hatua hiyo, iliyofikiwa na viongozi hao wawili, inatoa mwanya kwa uchaguzi mkuu wa ndani ya klabu hiyo wa kumpata Mwenyekiti na viongozi wapya wa klabu hiyo kufanyika.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents