Moto Hauzimwi
TECNO Spark 2

Viongozi Zanzibar Flava Unit wadaiwa kutafuna fedha za chama

Baadhi ya viongozi wa chama cha wasanii visiwani Zanzibar kijulikanacho kama Zanzibar Flavour Unit, wanadaiwa kutafuna fedha za chama hicho.

FB_IMG_1453230875650

Taarifa kutoka Zanzibar zinadai kuwa fedha hizo zilikuwa zitumike kwaajili ya kutengeneza video ya wimbo waliotengeneza.

“Juzi kati lilifichukaa lililokuwa limefichwa kuna baadhi ya wasani wameanza kufungiwa baada ya kushtukiziwa wamekiasi chama baada kukabidhiwa kwa studio yakatokezea makubwa kwa wasanii sababu ni kuna wasanii wametafuna mkwanja mrefu baada ya kupewa pesa na chama(milioni 3)kwaajili ya maandalizi ya video ya nyimbo waliotengeneza,” mmoja wa wajumbe wa chama hicho ameiambia Bongo5.

Amesema kutokana na hujuma hiyo mamlaka ya serikali inayosimamia muziki visiwani humo COSOZA imedai kuishughulikia.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW