Afya

Viribatumbo na vitambi tishio kwa wanawake Tanzania, Vyanzo vya tatizo hilo vyatajwa

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa, amesema viwango vya utapiamlo ikiwamo uzito uliozidi kwa wanawake wenye umri wa kuzaa vimeongezeka nchini na havikubaliki kimataifa.

Image result for waziri mkuu
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa

Waziri Majaliwa alitoa kauli hiyo jana Oktoba 3, 2019 alipokuwa akifungua mkutano wa sita wa mwaka wa tathmini ya lishe nchini.

Majaliwa amesema pamoja na tafiti kuonesha kupungua kwa viwango vya udumavu na upungufu wa damu, bado viwango vyake havikubaliki kimataifa na viwango vya utapiamlo vimezidi kuongezeka na pia havikubaliki kimataifa hususan uzito uliozidi kwa wanawake wenye umri wa kuzaa.

“Tuzingatie taratibu za kula, watu wanayo lugha ya kujivunia wanapokula kujichana, lakini kujichana huko kuna madhara, asubuhi unajaza vitu vyote mayai badala ya moja unaweka matatu, viazi, mihogo mwingine chips tena asubuhi anasema anashushia, lazima tujadili tupeane utaratibu na kuelimisha jamii ulaji wa vyakula,”ameeleza Waziri Mkuu, Majaliwa.

Kwa upande mwingine, Majaliwa amewataka watoa ushauri nasa pia kutoa elimu kwa wanawake wenye umri huo ili kupunguza matatizo yanayoweza kujitokeza na ni hatari kubwa kwa nchi kutokana na kukabiliwa na aina nyingine ya utapiamlo.

“Wale wenzangu wa vitambi kama mpo lazima mfanye mazoezi ili muweze kuondokana na vitambi kwa kuwa vina madhara yake,

Udumavu, utapiamlo mkali na wakadiri una athari kubwa kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano, tunatakiwa kuongeza jitihada mbalimbali katika kupambana na aina zote za utapiamlo ili kufikia viwango vinavyokubalika kimataifa,

Wadau waeleze vigezo vya kimataifa ambavyo vinapaswa kufikiwa. Matokeo ya utafiti yatupe chachu ya kukabiliana na tatizo la utapiamlo,“amesema Mhe. Majaliwa.

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile, alisema suala la vitambi na viribatumbo kwa wanawake nchini ni tishio kwasasa ambapo takwimu zinaonesha thelusi moja ya wanawake wanatatizo hilo.

Kubwa na la kutisha bado thelusi moja ya wanawake katika nchi yetu wanakabiliwa na tatizo la vitambi na viribatumbo na hili eneo linazidi kuongezeka,“amesema Ndugulile.

Dkt. Ndugulile amesema Tanzania imepiga hatua katika kupunguza udumavu kutoka asilimia 34.4 kwa mwaka 2015 na kufikia asilimia 31.8.

Ukondefu nao umepungua kutoka asilimia 4.3 na kufikia asilimia 3.5, upungufu wa damu kwa akina mama nao umepungua kutoka asilimia 45 na kufikia asilimia 29,“ameeleza Ndugulile.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents