Michezo

Virusi vya Corona kuzuia ‘game’ ya England na Italia, Chelsea kuwaweka sokoni wachezaji 8, Sturridge agoma kutua Aston Villa

FA inasubiri ushauri wa serikali kabla ya kuamua kuhusu uwezekano wa uwepo wa mechi ya kirafiki mwezi ujao kati ya England na Italia, kutokana na wasiwasi wa mlipuko wa virusi vya corona. (Evening Standard)

Kocha wa Chelsea Frank Lampard anajiandaa kuwauza wachezaji wanane, wakiwemo mlinda mlango wa uhispania, Kepa Arrizabalaga, 25, wachezaji wa nafasi ya kiungo ,Jorginho, 28, na Ross Barkley, 26. (Sun)

Kepa Arrizabalaga

Manchester United ilikosa nafasi ya kupata saini ya beki wa kushoto wa Bayern Munich Alphonso Davies, 19 kwa kitita cha pauni milioni 2 mwaka 2017. (Times, subscription required)

Machester City inafikiria kutoa ofa ya pauni milioni 30 ili kumnasa mchezaji wa nafasi ya ulinzi Mason Holgate, 23. (Mirror)

Mshambuliaji wa Tottenham na timu ya taifa ya England Harry Kane, 23, analenga kurudi mwezi Aprili baada ya kupona jeraha lake la kano (Sun)

Mshambuliaji wa zamani wa Liverpool Daniel Sturridge, 30, alikataa uhamisho kwenda Aston Villa wakati wa dirisha la usajili mwezi Januari kwa kuwa anataka kuisaidia Trabzonspor kufuzu ligi ya mabingwa. (Fanatik, via Sport Witness)Daniel SturridgeSturridge alifunga zaidi ya magoli 60 katika kipindi cha miaka sita alichochezea Liverpool

Mwanamasumbwi Tyson Fury amealikwa kuzungumza na kikosi cha Manchester United kuhusu safari yake mpaka kuwa bingwa wa WBC baada ya kumchapa Deontay Wilder. (Metro)

Mlinda mlango wa Ujerumani Loris Karius, 26, anaitaka Liverpool imuachie ili akajiunge na Besiktas ya Uturuki kwa mkataba wa kudumu.(Fotospor, via Turkish Football)

Everton ilikataa ofa ya Tottenham wakitaka kumsajili mchezaji wa nafasi ya ulinzi Michael Keane, 27, mwishoni mwa mwaka 2019. (Football Insider)Harry KaneHarry Kane (Kulia)

Ofa ya pauni milioni 11 ya Sheffield United iliyotangaza kwa ajili ya mlinda mlango wa Trabzonspor Ugurcan Cakir, 23, imekataliwa. (Fotospor, via Turkish Football)

Manchester United bado wana matumaini kuwa mchezaji wa timu ya taifa ya England kwa wachezaji wa umri wa chini ya miaka 20, kiungo Angel Gomes, 19, atasalia Old Trafford pamoja na kuwa mkataba wake utamalizika mwezi Juni. (Manchester Evening News)

Mchezaji wa nafasi ya ulinzi wa kikosi cha Napoli Kalidou Koulibaly, 28, aliyeripotiwa kwa muda mrefu kutakiwa na Manchester United, amenunua nyumba mpya ya thamani ya pauni milioni 3.4 jijini Paris, hatua iliyosababisha tetesi kuwa atahamia Paris St-Germain. (Star)KoulibalyKalidou Koulibaly anahusishwa na taarifa za kuhamia Paris St-Germain

Aston Villa inalenga kumnyakua kiungo wa Ufaransa na kikosi cha Marseille Morgan Sanson, 25, ikiwa watasalia ligi kuu msimu huu. (Le Phoceen, via Birmingham Mail)

Mshambuliaji wa Arsenal Alexandre Lacazette amesema beki wa kushoto wa washika bunduki hao Bukayo Saka, 18, ni mchezaji mdogo aliye bora zaidi katika ligi kuu. (Evening Standard)

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents