Visura washuka bondeni

Waandaji wa Face of Tanzania, Irene Kiwia na Nancy Sumari, wamepanda pipa jana na kuelekea nchini Afrika Kusini pamoja na washiriki watano waliyoingia katika nusu fainali ya shindano hili…

Visura


 


Waandaji wa Face of Tanzania, Irene Kiwia na Nancy Sumari, wamepanda pipa jana na kuelekea nchini Afrika Kusini pamoja na washiriki watano waliyoingia katika nusu fainali ya shindano hili. Lengo la safari ni kupata uzoefu kutoka kwa wanamitindo wa kimataifa.


 



Washirki hao ambao wapo safarini ni Edna Makanzo, Emmy Malau, Irene Shirima, Neshino Laizer pamoja na Yvone Joseph na hao ndio tano bora ya visura wa Tanzania waliotajwa katika hafla fupi iliyofanyika jumatatu mchana ndani ya hoteli ya Regency Park mitaa ya mikocheni.


 



Wakiwa wameshikilia hati zao za kusafiria kila mmoja alionekana kuwa na furaha kwani aliamini kuwa hakuachaguliwa kimakosa kuwa ni kutokana na kile ambacho aliwavutia wale waliomchagua kupitia kura zilizokuwa zikipigwa na watazamaji.


 



Washindi hao wamekwenda nchini Afrika Kusini ambako watakaa kwa muda wa siku tano, na huko watapata bahati ya kukutana na mamodo kibao akiwemo mtanzania mwenzetu mwanadada Hapiness Magessa pamoja na Kaone, halikadhalika watajipatia bahati ya kujifunza masuala tofauti yanayihusiana na uanamitindo.


 



Wanamitindo hao wanatarajia kupambana mara watakaporejea nchini April 26 ambapo watafanya fainali ambayo inasubiriwa kwa hamu kuona jinsi ambavyo mtu anajinyakulia donge nono la hatari, ndani ya ukumbi wa Ubungo Plaza.


 


Pata ujumbe fupi ya video kutoka visura kwa kubofya hapa


 


 

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents