Habari

Vita dhidi ya dawa za kulevya itasaidia kupunguza wafungwa magerezani – Mrema

Mwenyekiti wa bodi ya Parole, Augustine Mrema amesema kuwa vita dhidi ya biashara ya dawa za kulevya itasaidia kupunguza kwa wingi wa wafungwa magerezani kwakuwa watu wengi watakapoacha kujihusisha na biashara hiyo vitendo vya uhalifu navyo vitapungua.

Akitoa tathmini ya utendaji wa bodi hiyo jijini Dar es Salaam, Mrema ametoa wito kwa Watanzania wote kwa kutumia majukwaa mbalimbali kukemea matumizi na biashara ya dawa za kulevya .

Mrema alisema, “Wasiruhusu rais kushindwa hili au Makonda kushindwa hili, hatutakaa tuibuke tena ni kukamatia hapohapo kwahiyo watu wema wajitokeze katika hii vita wasimuachie rais peke yake wasimuachie Makonda na Simon Sirro, tujitokeze tuhakikishe huu mtandao unavunjwa.”

Aliongeza “Mimi nilikuwa napendekeza kwamba kila mkutano wa hadhara utakaofanywa na viongozi wa vyama wasiache hii agenda tukiendelea hivyo watashindwa, tumeona tu kelele kidogo dawa zimekosekana mtaani, Je tukikazana baada ya mwezi madawa yatakuwa ni historia, alihoji?”

By: Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents