Technology

VITA VYA KIBIASHARA: Huawei wafutiwa leseni ya Android na Google, Hili ni anguko kwa simu zao duniani

Kampuni ya Google imefuta rasmi leseni ya Android kwenye kampuni ya simu za mkononi ya Huawei kutoka nchini China.

Kwa mantiki hiyo, simu zote za Huawei hazitakuwa na uwezo wa kutumia huduma na bidhaa zote zinazotolewa na Google kupitia soko la Google Play Store ikiwemo YouTube na Gmail.

Kwenye taarifa iliyotolewa na Android, imeeleza kuwa watumiaji wa Huawei wa sasa wataendelea kupata huduma zote huku majadiliano kati ya serikali ya marekani na kampuni ya Huawei yakiendelea.

Imeelezwa kuwa matoleo mapya ya Android yatakayotoka kuanzia mwakani, hayatapatikana kwenye simu za Huawei hivyo watumiaji hawatapata huduma kama YouTube na Google Maps.

Taarifu hiyo imetoka ikiwa kuna mvutano mkali kati ya Rais Trump na Kampuni ya Huawei, ambapo Trump amekuwa akipingana na kampuni hiyo juu ya uingizaji wa bidhaa zake nchini Marekani, akidai hawajakidhi vigezo vya kufanya biashara nao.

Huawei ndio kampuni kubwa ya simu nchini China inayokuwa kwa kasi duniani, mwaka jana 2018 kimauzo duniani ilichukua nafasi ya pili ikiwa nyuma ya Samsung duniani kote.

Kwa upande mwingine, Huawei wametangaza kuja na mfumo wao mpya wa ‘HUAWEI HONGMEG OS’ ambao umeanza kufanya kazi nchini China pekee.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents