Michezo

Vita ya 16 bora kuikutanisha miamba ya soka leo, Ufaransa dhidi ya Argentina wakati Uruguay na Ureno

Michuano ya kombe la dunia inatarajiwa kuendelea hii leo siku ya Jumamosi kwa michezo miwili kupigwa kwenye viwanja tofauti ikiwa ni hatua ya 16 bora itakayo endelea huko nchini Urusi.

Majira ya saa 11 jioni timu ya taifa ya Ufaransa itakuwa na kibarua kizito cha kuikabili Argentina kuwania nafasi ya kutinga hatua ya robo fainali ya michuano hiyo mikubwa, mchezo huo unaotarajiwa kuwa na mvuto mkubwa hasa kwa vikosi vyote viwili kuwa na wachezaji nyota wanao kubalika na wapenzi wengi wa soka.

Ufaransa ikiongozwa na nyota wa Atletico de Madrid ya Hispania, Antoine Griezmann, Paul Pogba, Mbappe na wengine wengi kwa upande wa Argentina wao watakuwa na mchezaji bora duniani na kipenzi cha wengi wapenda soka, Lionel Messi anayekipiga FC Barcelona.

Na kunako majira ya saa 3 usiku Ureno itakuwa na kibuarua dhidi ya Uruguay mchezo utakao kuwa na msisimko mkubwa baada ya kuwakutanisha wachezaji wa klabu mbili hasimu nchini Hispania Real Madrid na Barcelona.

Cristiano Ronaldo ataongoza jahazi la Ureno kuhakikisha inapata ushindi pale atakapo kutana naLuis Suarez wa Barcelona ambaye naye akihitaji kuhakikisha Uruguay haipotezi mchezo huo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents