Michezo

Vita ya fedha Manchester City dhidi ya Paris St-Germain kunasa saini ya Boateng

Klabu ya Manchester City ya nchini Uingereza ipo kwenye vita kubwa dhidi ya matajiri wa Ufaransa timu ya Paris St-Germain kila moja ikijaribu kuwania saini ya beki wa Bayern Munich, Jerome Boateng.

Kwamujibu wa Sport Bild – Manchester Evening News,  Manchester City inavutiwa na Jerome Boateng na klabu ya Bayern Munich imejiandaa kusikiliza ofa itakayoletwa na mabingwa hao wa Uingereza kwaajili ya beki huyo ambaye kwa sasa yupo nchini Urusi kwenye michuano ya kombe la dunia.

Chanzo hicho kimeeleza kuwa Paris Saint-Germain nayo imeonyesha nia ya kumuhitaji mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 na hivyo City watalazimika kuchangamka ndani ya wiki hizi kama inamuhitaji kweli.

Mabingwa wa wa ligi ya Bundesliga wapo tayari kusikiliza ofa yoyote itakayo fika mezani kwao dau la kuanzia euro milioni 50 hadi 60.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents