Habari

Vita ya kibiashara kati ya Marekani na China yazidi kushika kasi, China yajibu mapigo

Vita ya kibiashara kati ya Marekani na China yazidi kushika kasi, China yajibu mapigo

China imesema italipiza kisasi kwa kutoza ushuru wa dola bilioni sitini kwa bidhaa za kutoka Marekani, baada ya rais Donald Trump kutangaza kiwango cha ushuru wa ziada kwa bidhaa zinazoingia kutoka China.

China ilitangaza hivyo baada ya kutangazwa kuwa ushuru wa ziada kuwa dola bilioni 200.Mvutano huu ni matokeo ya vita ya kibiashara kati ya nchi hizi mbili zenye uchumi mkubwa.Wizara ya fedha ya China imesema inalipiza kile alichokiita ajenda ya Marekani ya kutazama upande mmoja na biashara yenye ushindani usio wa usawa.

Rais Trump ametahadharisha kuwa atalipa kisasi ikiwa wakulima, wafugaji na wafanyakazi wa kimarekani watalengwa kwenye maamuzi ya China.Amesema milango iwazi iwapo China itataka kuzungumza.Trump amesema China imepatiwa fursa nyingi na sasa China inataka kufanya mazungumzo.

” Tumekuwa na biashara isiyo na uwiano sawa na China, mwaka jana tulipoteza kiasi cha zaidi ya dola bilioni mia tano kwa China, hatuwezi kufanya hivyo” Akizungumza mjini Beijing,msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China, Geng Shuang, amesema mazungumzo kati ya China na Marekani ni njia pekee ya kuondokana na mvutano huo.

”China imesisitiza kuwepo kwenye mazungumzo tena mazungumzo yenye usawa, kuaminiana na kuheshimiana ni njia pekee ya kumaliza mzozo wa kiuchumi na biashara kati ya China na Marekani.Marekani inachofanya hivi sasa hakionyeshi ukweli wala nia njema” Mickey Kantor alifanya kazi katika utawala wa Clinton kama waziri wa biashara wa Marekani.Ameiambia BBC kuwa ushuru uliowekwa na Rais Trump utakuwa hasara kwa Amerika.

”Itawaumiza watumiaji wa Marekani, itaathiri wafanyabiashara wanaotegemea bidhaa kutoka China kuendesha biashara zao, hakuna shaka kuhusu hilo na inawezekana hali hii inaweza kutuingiza kwenye kile watu wanachokiita vita ya kibiashara ambayo haitakuwa nzuri kwa yeyote.

Tunapaswa kufuata taratibu za biashara kimataifa, tunapaswa kushirikiana, tunapaswa kuondoa tofauti zetu katika meza ya mazungumzo”. Alieleza kiongozi huyo wa zamani.

Chanzo BBC

 

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents