Vita ya kuwania kiatu cha dhahabu Premier League
Vita ya kuwania kiatu cha dhahabu Premier League
Wakati bingwa wa Premier League akiwa tayari ameshajulikana, vita pekee kwenye ligi hiyo pendwa ulimwenguni imehamia kunako kiatu cha dhahabau ‘Golden Boot’.
1. Jamie Vardy – magoli 19
Mshambuliaji wa klabu ya Leicester City, Jamie Vard anaongoza kwenye mbio za kuwania kiatu cha dhahabu kwa kufanikiwa kufunga jumla ya magoli 9 mpaka sasa kunako Premier League.
Kama atafanikiwa kuongoza mpaka mwishoni mwa ligi nyota huyo wa Foxes’ mwenye umri wa miaka 33 atakuwa amejinyakulia kiatu hicho cha Golden Boot kwa mara ya kwanza kunako Premier League.
2. Danny Ings – magoli 18
Nyota huyo wa zamani wa Mabingwa wapya wa Premier League Liverpool anaufurahia vema msimu wake Southampton kwa kufanikiwa kufunga jumla ya mabao 18 na hivyo kushika nafasi ya pilikwenye mbio za kinyang’anyiro hicho cha ufungaji bora.
3. Mohamed Salah – magoli 17
Mshambuliaji wa Liverpool ambaye alifanikiwa kumaliza msimu wa ligi wa 2017-18 kwa kufunga magoli 32 na kuungana na Aubameyang pamoja na Mane, Mohammed Salah sasa anashika nafasi ya tatu kwenye mbio hizo akiwa na magoli 17.
3. Pierre-Emerick Aubameyang – magoli 17
Kwenye nafasi hiyo ya tatu yupo pia nyota wa klabu ya Arsenal , Aubameyang ambaye mpaka sasa na yeye ameshafumania nyavu mara 17.
5. Sergio Aguero – magoli 16
Nyota wa Manchester City, Sergio Aguero anaingia kwenye mbio hizo akiwa na magoli yake 16, mabao hayo ameyafunga kwenye michezo yake 24 aliyocheza.
6. Sadio Mane – magoli 15
Kama kawaida Liverpool imefanikiwa kumuingiza tena Sadio Mane kwenye mbio hizo za kiatu cha dhahabu kwa kufanikiwa kufunga magoli 15 mpaka sasa.
6. Raul Jimenez – magoli 15
Klabu ya Wolves imefanikiwa kumuingiza mchezaji wao raia wa Mexico, Raul Jimenez katika kinyang’anyiro hicho baada ya kutupia jumla ya magoli 15 mpaka sasa.
8. Marcus Rashford – magoli 14
Licha ya kusumbulkiwa na majeraha nyota wa Manchester United, Marcus Rashford amefanikiwa kufunga jumla ya magoli 14 na hivyo kuingia kwenye mbio hizo.
8. Anthony Martial – magoli 14
Mshambuliaji wa Man United, Mfaransa Anthony Martila ameungana na mchezaji mwenzake Rashford katika kinyang’anyiro hicho cha kuwania kiatu cha dhahabu kwa kufunga jumla ya magoli 14.
Imeandikwa na Hamza Fumo