DStv Inogilee!

Vitendo vya ubaguzi vyamkosesha dili mchekeshaji Kevin Hart tuzo za Oscar

Mchekeshaji maarufu duniani kutoka pande za Marekani Kevin Darnell Hart alimaarufu Kevin Hart, aliyezaliwa miaka 39 iliyopita katika mitaa ya Philadelphia, Pennsylvania, amekosa dili kutokana na vitendo vya ubaguzi.

Mchekeshaji huyo ambaye amekuwa mara kwa mara akipata madili mengi ya kuhost show mbalimbali zikiwemo za BET na nyinginezo nyingi mara hii dili la kuhost katika ugawaji wa tuzo za Oscar 2019 limeyeyuka kutokana na vitendo vya ubaguzi kwa watu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja.

Mapema mchekeshaji huyu alitoa taarifa kuwa atakuwa host siku hiyo ya ugawaji wa tuzo hizo,lakini kupitia ujumbe alioupost kwenye akaunti zake za mitandao ya kijamii ameamua kujivua nafasi hiyo.

Hii imekuja baada ya wasakuzi wa mitandao ya kijamii kubaini kuwa mchekeshaji huyu aliwahi kutweets mnamo mwaka 2010 zilikuwa zikitoa maneno ya kashfa na kibaguzi kwa watu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja  (LGBT Community).

Usiku mtandao wa tweeter uliibuka na kuanza kumshsmbulia Kevin Hart kutokana na kauli zake hizo alizowahi kuzitoa hadi kufikia jamaa kuona basi isiwe kesi acha nifunguke, na kufunguka kwake aliamua kujitoa au kujivua kwenye nafasi hiyo amabyo ilikuwa kama ndoto yake ya muda sasa, ambayo ilikuwa ni kuwa host katika siku ya ugawaji wa tuzo za Oscar 2019, na kubaini kuwa ” Asingekuwa kikwazo cha furaha za watu siku hiyo ya utoaji tuzo endapo watu wakimuona”

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW