Tupo Nawe

”Vitu anavyo fanya Messi, utaviona kwenye ‘Playstation’ Tu,”-Gattuso awapa onyo Napoli

Kocha wa Napoli, Gennaro Gattuso amewasisitiza vijana wake kujiandaa vema dhidi ya mshambuliaji hodari na bora duniani, Lionel Messi kwa kuwa vitu anavyo vifanya kiumbe huyo uwanjani utaweza kuviona kwenye ‘Playstation’ pekee na si kwingineko.

Image result for messi skills

Gattuso na kikosi chake kitawakaribisha miamba hiyo ya soka ya Catalan katika dimba la San Paolo siku ya Jumanne lakini Bosi huyo wa Napoli ameonya kuwa wapo tayari kumzuiya Messi na wachezaji wengine wa Barcelona kuchomoza na ushindi siku hiyo.

Napoli kwa mara ya tatu wanatinga hatua hiyo ya 16 bora ya Champions League na inakutana na mlima mkubwa wa kupanda ili kusonga mbele.

”Ni lazima tucheze bia hofu, nataka kuona namna timu itakavyo pambana, Messi yupo vizuri sana anaweza kufanya kitu ambacho unaweza kuona kwenye ‘Playstation,’ pekee lakini lazima tujitahidi kumzuia.” amesema Gattuso

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW