Bongo5 Makala

Vitu vitano kutoka Fresh Remix, je Diamond kawachana Alikiba na Hamisa Mobeto?

Siku ya jana August 21, 2017 msanii wa muziki wa hip hop Bongo, Fid Q alitoa surprise ya aina yake kwa mashabiki wake kwa kuachia remix ya ngoma ‘Fresh’ ambapo ndani yake amewashirikisha Diamond Platnumz na Rayvanny, wote kutoka WCB.

Katika ngoma hii yenye dakika tatu na sekunde nane wasanii wote wameshusha michano ya uhakika huku Fid Q akianza verse ya kwanza, Dimond ya pili kisha Rayvanny na Fid Q kurudia tena.

Naomba nijikite katika verse ya pili ya Diamond ambayo ukiisikiliza kwa makini utagundua amezungumza mambo mengi yenye uzito ila ni vigumu kupata jumbe huo moja kwa moja kwa kuwa ametumia zaidi lugha ya sanaa.

Kwa ufupi haya ni mambo matano ambayo nimewaza kuyabaini katika verse hiyo.

  1. Kufanya muziki wa Rap

Hapo awali kabla ya kutoka Diamond alikuwa akifanya muziki wa rap, kama ni mfuatiliaji mzuri wa muziki utakuwa umesikia baadhi ya nyimbo zake za awali akirap ambazo mojawapo alifanya kwa producer Lamar.

Hivyo kupita ngoma hii ya Fid Q si bahati mbaya ni kitu ambacho anakijua na alichokifanya ni kizuri pia.

Kusikia beat tu nikatamani nifanye verse, nikamcheki Ngosha akaniambia Simba mbona fresh.

Upesi upesi nikaandika ni-murder kesi, sasa ngoma kitaani imenuka kama kinyesi.

Hizo ni line alizoanza nazo katika ngoma hiyo, ikumbukwe mwaka 2014 Diamond alitoa ngoma na rapper Godzilla pamoja na Zachaa iliyotiwa Mtoto wa MamaPia aliweza kupitia vizuri katika beat ya Fat Joe ‘All The Way Up’

  1. Hustle zake/mapenzi

Pia Diamond ameweza kukumbushia hustle zake kabla ya kutoka na kuwa msanii maarufu na tajiri na namna watu walivyokuwa wakichukulia muonekano wake kwa wakati huo.

Am still young kabla sijaitwa Chibu Denga, enzi hizo naitwa domo sasa hivi eti lips denda, fresh

Pengine hiki ni kitu ambacho kilimuumiza sana kwa wakati huo hasa linapokuja suala la warembo lakini baada ya kupata umaarufu na fedha ikawa siyo tatizo tena kila mrembo alichukulia hilo kawaida.

Ni kitu ambacho katika ngoma yake na Nay wa Mitego ‘Mapenzi Pesa’ pia walikizungumzia.

  1. Moto wa Hamisa Mobetto

Moja ya stori ambazo zinasambaa kwa sana kwa sasa kuhusu Diamond ni madai ya kuza na model na video vixen, Hamisa Mobetto.

Kipindi cha ujauzito wa mrembo huyo ambaye alitokea katika video ya Diamond ‘Salome’, tetesi zilikuwepo tu, ila baada ya Hamisa kujifungua mtoto wa kiume na kumpatia jina la ambalo ni sawa na ile la Diamond yaani Abdul Naseeb ndipo maneno yakawa mengi.

Baba Tiffah ama niite baba Nillan, nasikia naitwa baba Abdul kuna mambo mitaani, fresh.

Bado ni vigumu kusema moja kwa moja ujumbe huu umemlenda Hamisa Mobetto. Itakumbukwa wiki iliyopita Diamond aliandika ujumbe wenye utata katika mtandao wa twitter ambo ulidaiwa kumlenga mrembo huyo.

4.   Biashara zake

Msanii yeyote ambaye ana nia ya kufika mbali hujikita kuwekeza katika muziki wake na kufanya biashara nyingine. Leo hatumsikii sana P Diddy katika muziki lakini ni vigumu kumkosa katika orodha ya wasanii matajiri Marekani, kisa ni biashara.

Diamond naye yupo katika utaraibu huo, tumeona akiingiza sokoni manukato yake ‘Chibu Perfume’ na Karanga kitu ambacho anajivunia popote aendapo.

Mzuka ukipanda ukate viuno kama vanga, beat ya kubanda inayokabwa na muuza karanga, fresh

Hii inaonyesha ni kwa namna gani anavyopenda biashara yake na haoni aibu kijisifia kwa hatua hiyo aliyofikia.

  1. Kuhusu Alikiba

Kwa sasa katika muziki wa Bongo Flava Diamond na Alikiba wanatajwa kama washindani wakubwa, achilia mbali madai ya kuwepo kwa beef kati yako. Hawa katika Bongo Flava ni kama Simba SC Vs Yanga SC au FC Barcelona na Real Madrid pale Spain, weka nukta hapo.

Katika ngoma hii kuna line ambazo hazijaeleweka zinamlenga nani ili ukichukua matukio ya nyuma kuna uwezekano ikawa ni Alikiba. Narudia tena, kuna uwezekano!!, kwa maana kwamba inaweza kuwa ndivyo au sivyo.

Ukinichukia sikosi hela, kuni-compare na cinderella haiwezi kuwa fresh

Simba kutoka mbuga ya Tandale, naona swala wanaforce tuwe sare sare,

Viuno vidogo wanataka pensi ya Pepe kale, siwalitaka kiti nimewapa hadi kitanda wakalale,

Katika lines hizi za mwisho kuna mambo mawili, mosi; utakumbuka wimbo wa kwanza kumtoa Alikiba kimuziki ni Cinderella, hivyo unachukua mstari tajwa hapo juu na kulinganisha na hili unagundua jibu lake bado lina fumbo ndani yake.

Pili; wakati Alikiba anatangaza ujio mpya mwaka 2014 kupitia wimbo wa Mwana baada ya ukimya wa muda mrefu, alidai nafasi/kiti chake kipo bado katika muziki ila kina vumbi tu, hivyo kazi anayotakiwa yeye kufanya ni kufuta vumbi na kuendelea kukaa kama mfalme wa Bongo Flava.

By Peter Akaro

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents