Moto Hauzimwi
TECNO Spark 2

Vitu vitatu vilivyomvutia Professor Jay kwenye harusi yake

Baada ya kufunga pingu za maisha na mchumba wake siku Grace, msanii hip hop Bongo Professor Jay ametaja vitu vitatu vilivyomvutia kwenye harusi yake.

Rapper huyo mkongwe na Mbunge wa Mikumi, ametaja vitu hivyo kuwa ni ushirikiano na wasanii wenzake, uwepo wa media na kuunganisha viongozi mbali mbali wa kisiasa.

“Chakwanza ni support kubwa ya watu wangu wa mtaa, nikaona watu wote wapo pale especially wasanii wenzangu walikuwepo sana sana, wengine walishindwa kuja kwa sababu mbali mbali,” ameiambia FNL ya EATV na kuendelea.

“Pili media ime-play part yake vizuri sana, lakini kikubwa mbacho namshukuru Mwenyenzi Mungu mbele za haki nimejitahidi hata kuungainsha siasa zetu za Tanzania. Viongozi wote waliopata kuongea  walisema huyu jamaa ametuunganisha, watu wa vyama vyote walikuwa pale, watu wa dini zote walikuwepo pale, ni kitu kikubwa namshukuru Mungu,” amesema Professor Jay.

By Peter Akaro

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW