Siasa

Vituko vya marais mkutano wa SADC

MKUTANO wa wakuu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) uliomalizika jana, uliambatana na matukio mbalimbali ya hapa na pale.

Oscar Mbuza

 

MKUTANO wa wakuu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) uliomalizika jana, uliambatana na matukio mbalimbali ya hapa na pale.

 

Tukio la kwanza lilikuwa ni kwa Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe ambaye pamoja na kugoma kujibu maswali mengi ya waandishi wa habari alipokuwa akiingia katika Hoteli ya Kilimanjaro Kempinski, alishindwa kujizuia kujibu swali aliloulizwa kuhusu hali yake ya afya.

 

Huku akionekana kutokuwa mkakamavu kama kawaida yake, Rais Mugabe (83), alisisitiza kwamba afya yake ni njema na kuongeza kuwa ana nguvu za kutosha. “Sijambo nina nguvu za kutosha,” Rais Mugabe alijibu kwa kifupi na kuingia hotelini.

 

Rais Mugabe alikuwa kiongozi wa mwisho kuwasili hotelini hapo, akisindikizwa na lundo la askari kanzu na kupelekwa moja kwa moja kwenye chumba cha mkutano. Rais Levy Mwanawasa wa Zambia alitoa kituko kwa kumuonyeshea ishara ya kumtaka kufumba mdomo mwandishi wa habari aliyekuwa akimuuliza kiini cha kuitishwa kwa mkutano huo wa dharura wa SADC.

 

Kwa upande wake Rais Jakaya Kikwete, yeye pia pamoja na kukataa kujibu maswali ya waandishi wa habari alipokuwa akiingia hotelini hapo, alijikuta akishindwa kujizuia baada ya kuulizwa kama mkutano huo ulitokana na shinikizo fulani.

 

“Tunakwenda kwenye mkutano, shinikizo …. shinikizo gani unalosema wewe,” alisema Rais Kikwete na kuingia hotelini tayari kwa kikao hicho. Huku akionekana kutokuwa mkakamavu kama kawaida yake, Rais Mugabe (83), alisisitiza kwamba afya yake ni njema.

 

Source: Habri Leo

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents