Habari

Vituo viwili vya TV Kenya vimewaachisha kazi wafanyakazi wake zaidi ya 100 ndani ya mwezi mmoja, kimoja chafungwa!

Kituo cha runinga nchini Kenya Kiss TV kinachomilikiwa na Radio Africa Group kimewaachisha kazi wafanyakazi wake zaidi ya 27 kutokana na kujiendesha kwa hasara toka mwezi (March) mwaka huu.

Kiss TV

Kwa mujibu wa CEO Patric Quarcoo, kituo hicho kimekuwa kikipata hasara ya shilingi ya Kenya M 10 (zaidi ya M 180 Tshs) kila mwezi toka March mwaka huu.

Taarifa kutoka mitandao ya Kenya zinasema kati ya wafanyakazi waliopoteza kazi ni pamoja na wale wa kitengo chote cha habari.

Taarifa nyingine iliyopatikana kutoka katika nyaraka za siri za kampuni hiyo zilizovuja siku za hivi karibuni, zilionesha mipango ya kituo hicho kufunga kabisa idara ya habari ya kituo hicho na badala yake kuja na kituo mbadala cha muziki na burudani pekee. Kwa mujibu wa Ghafla, kituo kipya cha burudani na muziki kinachotarajiwa kuzinduliwa hivi karibuni kuchukua nafasi ya Kiss kitaitwa Blaze TV.

k24 billboard

Mwanzoni mwa mwezi huu kampuni nyingine ya MediaMax ya nchini humo iliwaachisha kazi zaidi ya wafanyakazi 70 kwa sababu zinazofanana na zile za Kiss TV, za kujiendesha kwa hasara.

Wafanyakazi waliopoteza kazi katika kampuni hiyo ni pamoja na wale wa upande wa kituo cha Televisheni K24, na vituo viwili vya radio vinavyomilikiwa na kampuni hiyo Kameme FM na Milele FM.

Kati ya watangazaji na waandishi waliopoteza kazi ni pamoja na wale ‘bora’ waliochukuliwa kutoka katika vituo vingine kwa ahadi za mishahara minono wakati wa kuanzishwa kwake.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents