Habari

Vivazi vya Barron Trump vyazua kasheshe

Vivazi vya mtoto wa Donald Trump, Barron Trump amejkuita akishambuliwa katika mtandao wa Twitter kutokana na vivazi vyake amabvyo vinapingwa kuwa havifanani na hadhi ya baba yake na mama yake.

Famila ya Rais Donald Trump( Kushoto), Barron Trum( kati) na Melania Trump( Kulia)

Hata hivyo Barron amejikuta akitetewa na Chelsea Clinton, mtoto wa Rais wa zamani wa Marekani katika mtandao huo kwa mavazi yake.

Gazeti la The Daily Caller, lililipoti siku ya jumatatu kuwa mavazi ya kijana huyo wa miaka 11, yamekuwa hayaendani na heshima ya Ikulu ya nchi hiyo. Baada ya kupokea mashambulizi hayo na kutetewa mama wa kijana huyo Melina Trump alimshukuru binti wa Clinton. Awali Clinton aliwahi kumtetea Barron aliposhutumiwa na kukosolewa na hata kufanyiwa utani.

Na Laila Sued

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents