Mitindo

Vivazi vya Michelle Obama vyazidi kupagawisha

Kwa siku mbili mfululizo nchini Italia hususani katika mji wa Tuscany, wanazidi kuiona joto ya mitindo kutoka kwa mke wa Barrack Obama,Michelle Obama kwani amegeuka gumzo kwa jiji hilo kwa kupagawisha watu na mitoko yake ya kijanja.

Mke huyo wa Rais wa zamani wa Marekani siku ya jumapili(juzi) alionekana akizunguka katika maeneo ya Montalcino, huku akiwa amevalia blauzi yake ya pinki ilioacha bega moja wazi na jeans nyeupe, basi mji huo na dunia ya mitindo macho yote yalikuwa kwa mwanamama huyo alivyotupia na kupendeza.

Kwa siku ya jana Michelle na mumewe walizidi kuinyanyua midomo ya wapenda mitindo pamoja na wakazi wa mji huo kwa muonekano wao casually huku Obama yeye akivaa shati refu lililokunjwa na kuvalia suruali likifanana na lenal, na mkewe alivyaa blauzi nyeupe ya kuacha mabega wazi pamoja na suruaji mithiri ya lenal ya kijani kibichi.

Wawili hao huku wakiwa wameambatana walinzi wao walionekana wakitembea pamoja katika mji huo na kuacha gumzo kwa kupendeza sana kutokana na uvaaji wao.Obama na mkewa kwa sasa anatumia muda wake kupumzika nakutuliza akili.

Na Laila Sued

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents