Promotion

Vodacom Miss Tanzania 2007

Richa AdhiaRicha Adhia ndiye mshindi wa Vodacom Miss Tanzania 2007, mshindi wa pili ni Lilian Abel ambaye kama Richa ametokea wilaya ya Kinondoni. Mshindi wa tatu ni Queen David ambaye ni Miss Temeke.

Richa Adhia

 

Richa Adhia ndiye mshindi wa Vodacom Miss Tanzania 2007, mshindi wa pili ni Lilian Abel ambaye kama Richa ametokea wilaya ya Kinondoni. Mshindi wa tatu ni Queen David ambaye ni Miss Temeke.

 

Taji la Redds Ambassador (balozi wa redds) limenyakuliwa na Victoria Martin ambaye ni Miss Tanga na Miss Kanda Kaskazini.

 

Hii ni mara ya kwanza tangu Miss Tanzania ifufuke mwaka 1994 kwa mtanzania mwenye asili ya kihindi kunyakua taji hilo.

 

MRATIBU wa shindano la Vodacom Miss Tanzania, Hashim Lundenga amesema haoni tatizo kwa Richa Adhia kuwa Miss Tanzania licha ya kuwa mwenye asili ya kihindi.

 

Lundenga alisema kuwa mashindano ya Miss Tanzania, hayana mipaka kwa watu ambao ni Watanzania halisia na kwamba wote wana nafasi sawa kushiriki.

 

“Unajua kila kitu kizuri kitakuwa na kukosolewa, kila kitu kizuri hakikosi lawama, sasa sisi tunasema kama Kamati ya Miss Tanzania, msichana yeyote mwenye sifa na ni Mtanzania hata awe mzungu, madam ni Mtanzania ana nafasi ya kushiriki,” alisema Lundenga.

 

Katika shindano hilo lililofanyika kwenye Viwanja vya Leaders, Kinondoni, Richa Adhia alitwaa taji na kuondoka na gari aina ya Toyota RAV4 la sh45mil, sh8mil na vidani na hereni vyenye thamani ya sh4m pamoja na tiketi ya kuiwakilisha Tanzania katika shindano la urembo la dunia.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents