Promotion

Vodacom waizindua 3G ndani ya Sullivan

logo-vodacom.png Kampuni ya Vodacom Tanzania imezindua huduma yake ya 3G mkoani Arusha ambayo itawawezesha wateja kupata huduma ya uhakika na haraka ya mtandao katika Mkutano wa nane wa Sullivan unaoendelea.

logo-vodacom.png

Kampuni ya Vodacom Tanzania imezindua huduma yake ya 3G mkoani Arusha ambayo itawawezesha wateja kupata huduma ya uhakika na haraka ya mtandao katika Mkutano wa nane wa Sullivan unaoendelea.

Akizungumza na Waandishi wa Habari, Mkurugenzi wa Masoko wa Vodacom Tanzania, Bw. Ephraim Mafuru alisema huduma hiyo imezinduliwa sambamba na mkutano wa Sullivan ulioanza Jijini Arusha.

Aidha Bwana Mafuru, alisema huduma hiyo inazinduliwa Jijini Arusha baada ya kuzinduliwa katika Jiji la Dar es Salaam na Dodoma, mapema mwaka huu.

Alisema mbali na kuiwezesha Intaneti kuwa na nguvu pia wateja wawili wanapokuwa na simu zenye viwango vya huduma hiyo wanaweza kuonana moja kwa moja wakati wanawasiliana. Alisema Vodacom Tanzania, itaendelea kuisambaza huduma hiyo sehemu mbalimbali katika Tanzania na kwamba huduma hiyo ni chachu ya kuleta maendeleo nchini.

Bw. Mafuru, aliongeza kuwa Vodacom Tanzania imejizatiti kuhakikisha kwamba Watanzania wengi kadri iwezekanavyo wanafaidika na huduma hiyo na kwamba, huduma nyingine zitafuata mbali na hii ya 3G iliyozinduliwa jana.

Kuhusu faida ya huduma hiyo katika mkutano huo, Mafuru alisema 3G itawaunganisha wajumbe wa mkutano huo na dunia kwa kuwa inaiwezesha Intaneti kuwa na kasi na nguvu kubwa, anasema katika bara la Afrika Tanzania ni nchi ya pili kuwa na huduma hiyo baada ya Afrika Kusini.

“Ukweli ni kwamba tumedhamiria kulifanya suala la mawasiliano baina ya wajumbe wa Arusha na kote Duniani kuwa rahisi na jepesi kulingana a ukuwaji wa teknolojia”

Alisema. Huduma nyingine inayotolewa na Vodacom ni ya M-PESA ambayo alisema inawawezesha wateja wa Vodacom kutuma Pesa kwa wapendwa wao kwa kutumia simu iliyoko kiganjani tu.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents