Michezo

Vunja mchezo endapo Mashabiki watatoa Lugha za kibaguzi-FIFA

Mashindano makubwa ya Mabara yanatarajiwa kuanza kutimua vumbi jumamosi ya wiki hii nchini Urusi na hii ikiwa ni kabla ya mwaka mmoja kufanyika kwa fainali za kombe la dunia.

Kuelekea Michuano hiyo Shirikisho la mpira wa miguu ulimwenguni (FIFA) limewataka waamuzi wote watakochezesha kuvunja mchezo endapo Mashabiki watatoa Lugha za kibaguzi wakati wa Mechi.

Matatizo ya kibaguzi katika michezo imekuwa ni jambo linalopigwa vita licha ya Urusi ambao ndio wenyeji wa fainali za kombe la Dunia za Mwaka 2018, kuwa miongoni mwa mataifa yanayo ongoza katika jambo hilo, hivyo FIFA imedai kuwa itaweka waangalizi wa mambo ya kibaguzi viwanjani.

Katika kundi A linalo ongozwa na mwenyeji Urusi kuna timu za New Zealand, Ureno pamoja na Mexco, ambapo katika mchezo wa ufunguzi Urusi itakabiliana na New Zealand.

BY HAMZA FUMO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents