Habari

Vyombo vya dola vina uwezo wa kutoa uchunguzi tukio la Mh. Lissu – Waziri Mkuu

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema kuwa wao kama serikali wanaamini kuwa vyombo vya dola vina uwezo wa kutoa uchunguzi wa tukio la kushambuliwa kwa risasi kwa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu na kama wataona kuna umuhimu wa kuhitaji wachunguzi kutoka nje vyombo hivyo vyenyewe vinaweza vikachukua hatua vikalieleza jambo hili na si yeye.

Waziri Mkuu ameyazungumza hayo leo bungeni mjini Dodoma baada ya Kiongozi wa Kambi rasmi bungeni, Freeman Mbowe kuhoji kuwa tukio la kushambuliwa kwa Mbunge huyo ni tukio kubwa hivyo basi tukio hilo halipaswi kuchanganywa na mengine, Je,? Serikali inaona nini kutafuta wachunguzi kutoka nje kuja kufanya uchunguzi wa jambo hilo?

“Hakuna mtu aliyefurahishwa na tukio alilofanyiwa mbunge mwenzetu hakuna mtu anaefurahishwa na mambo yanayojitokeza huko yawe ya mauaji yawe ya mashambulio au migongano inayoendelea kwenye jamii yetu, lakini vyombo vya dola tumevipa jukumu la kusimamia kulinda jukumu na kulinda usalama wa raia na mali zao kwa kiwango kinachotakiwa, na pale ambako kuna tokea tazito vyombo vya dola vinajukumu la kuhakikisha vina fanya uchunguzi kuwakamata wale wote ambao wamehusika, lakini mimi nimeeeleza hapa watu wote watenda makosa yale ni watu ambao wamejiandaa kuficha uovu wao dhidi ya vyombo vya dola na si kwamba vyombo vyotee vya dola havina uwezo wa kufanya yake kiuchunguzi na mimi nakuhakikishia hayo matukio yaliyojitokeza wanayo mengi,” amesema Majaliwa.

“Kila mmoja ashiriki katika kutoa taarifa sisi tunakaribisha mtu yoyote anayejua kuna muelekeo atusaidie ili vyombo vya dola viweze kufanya kazi yake kwa urahisi zaidi, kwahiyo najua unazungumzia kwa upande wako kama kiongozi wa Kambi rasmi ya upinzani bungeni tunajua kuwa Tundu Lissu ni mbunge anaetoka upande wako lakini na sisi ni mbunge mwenzetu pia lazima tushirikiane kuhakikisha jambo hili linapata muelekeo kwahiyo nikuhakikishe vyombo vyetu uwezo upo lakini pale ambapo tutaona kama kuna umuhimu huo vyombo vyenyewe vinaweza vikachukua hatua vikalieleza mimi siwezi kulihakikishia taifa kwamba tumekosa uwezo kwasababu tunaamini vina uwezo wa kutoa uchunguzi kwahiyo kiongozi mwenzangu wa Kambi ya upinzani naomba uamini kwamba serikali yetu inayo nia njema familia ya watu wote walioathirika wakiwemo wa familia ya Mbunge mwenzetu Tundu Lissu inayo nia njema ya kukamata lakini pia ya kulinda amani ya nchi hii ili kila mmoja hata sisi pia tuwe na uhakika wa shughuli tunazozifanya kila siku kwahiyo tutaendelea kufanya hilo na tutaendelea kuwasiliana kama kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani bungeni.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents