BurudaniHabari

Wa Project Fame kuondoka leo

Tusker Project FameWAWAKILISHI wanne wa Tanzania katika shindano la Vodacom Tusker Project Fame, wanatarajiwa kuondoka leo kwenda Nairobi, Kenya kwa ajili ya maandalizi ya shindano hilo litakalowahusisha pia washiriki kutoka nchi za Uganda na Kenya.

Tusker Project Famena Dina Zubeiry

WAWAKILISHI wanne wa Tanzania katika shindano la Vodacom Tusker Project Fame, wanatarajiwa kuondoka leo kwenda Nairobi, Kenya kwa ajili ya maandalizi ya shindano hilo litakalowahusisha pia washiriki kutoka nchi za Uganda na Kenya.

Washiriki watakaowakilisha Tanzania ni pamoja na Makaaya Sumari (24) ambaye ni dada wa Miss World Africa mwaka 2005, Nancy Sumari; Dominicina Richard (22), John Kimati (22) na Margaret Byamungu (21).

Meneja Masoko wa bia ya Tusker, Jemimah Gakuya, alisema jana jijini Dar es Salaam kwamba jumla ya washiriki, wanne kutoka kila nchi watakaa katika jumba litakaloitwa Project Fame kuanzia Oktoba 29 mpaka Desemba 17 ambako watakuwa wakionyesha vipaji vyao vya sanaa pamoja na kupatiwa mafunzo maalumu ya fani hiyo.

Aidha, katika jumba hilo wasanii hao watakuwa wakionekana kila wanachofanya kupitia televisheni ambako watazamaji watapata fursa ya kumpigia kura kila wiki msanii atakayeonekana hafai mpaka atakapobaki mshiriki mmoja atakayekuwa mshindi.

Mshindi huyo atajinyakulia gari mpya aina ya Mercedes Benz yenye thamani ya sh mil. 60 pamoja na mkataba wa kurekodi muziki na Kampuni ya Galo/Johnic na zawadi nyingine ikiwamo promosheni ya muziki wake.

Shindano la Vodacom Tusker Project Fame ni mchanganyiko wa mashindano ya Big Brother Africa na Pop Idol. Linaandaliwa na Kampuni ya Endemol kwa kushirikiana na Multichoice Africa.

Source: Tanzania Daima

{mos_sb_discuss:14}

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents