Habari

Waalgeria kupiga kura ya maoni mabadiliko ya katiba

Raia wa Algeria watapiga kura ya maoni leo kuhusiana na mapendekezo ya mabadiliko ya kikatiba ambayo upinzani unasema yatasaidia kuupa nguvu udikteta.

Algeria votes on tweaked constitution aimed at ending protest movement -  France 24

Kura hiyo inakuja karibu miezi 19 baada ya maandamano makubwa yaliyompelekea rais wa muda mrefu wa nchi hiyo Abdelaziz Bouteflika kuachia ngazi.

Rais Abdelmadjid Tebboune ambaye kwa sasa anapokea matibabu nchini Ujerumani aliahidi kuifanyia mabadiliko katiba baada ya kuchaguliwa kwake mwezi Disemba ingawa waandamanaji wamesema kuwa mabadiliko hayo si ya kidemokrasia.

Mabadiliko hayo yanampa rais uwezo wa kuhudumu kwa kipindi cha mihula miwili ya miaka mitano na mamlaka ya kumchagua Waziri Mkuu kutoka kwa chama cha walio wengi bungeni.

Ingawa wanaounga mkono wanasema mabadiliko haya yanaonyesha Algeria mpya wakosoaji wanaonya mamlaka haya yanakwenda kinyume na ahadi ya Tebboune ya kuondoa udikteta nchini humo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents