Michezo

Waamuzi wazikimbia mechi za Ligi Kuu, Mtendaji Mkuu TFF, Kidao afunguka ”Wiki hii tu, 7 wameomba wasipangwe, ni woga na presha”

Mtendaji Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Kidao Wilfred amesema kuwa jumla ya Waamuzi saba (7) wameomba kutopangwa kwenye ‘game’ za Ligi Kuu licha yakutofanya makosa yoyote yale huku akiamini ni kutokana na presha iliyopo kwa sasa na pengine wameingiwa na woga, na hivyo wanajaribu kuwatengeneza kisaikolojia ili kujiamini na kujuwa kuwa wanapopewa mechi ya kusimamia wajue wanadhamana kubwa.

Image result for Kidao Wilfred

Kidao ameyasema hayo hapo jana siku ya Jumamosi kwenye Mkutano wake na Waandishi wa Habari wakati akimtangaza Almas Kasongo kuwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi akichukua nafasi ya Boniface Wambura aliyemaliza muda wake.

”Wiki hii tu, kuna waamuzi saba (7) wameomba wasipangwe kwenye mechi za Ligi Kuu, hawajafanya makosa na hawajaaribu chochote. Lakini kwa maana ya presha ambayo imekuwepo waamuzi saba wote wametoa hudhuru.” Amesema Mtendaji Mkuu wa TFF, Kida0

Kidao Wilfred ameongeza kuwa ”Unaona sasa ni woga, lakini bilashaka sisi tunafanya kazi kubwa kuwaondoa kwenye uwoga. Bilashaka ukipewa nafasi ya kusimamia mechi ni dhamana kubwa uliyonayo. Jambo kubwa ni kuongeza umakini na kujiamini.”

”Kwa hiyo ni kuwatengeneza kisaikolojia kwamba ni kazi nzuri, kubwa na ukiaminiwa maana yake sio jambo dogo. Kwa hiyo nyie mna kalamu zenu, mnacho cha kusemea, mnaweza mkasema watu wakawasikiliza. Vyombo vya habari vinanguvu kubwa, wakati tunakwenda kuchambua, tuchambue maana ya kujenga.”

Mtendaji huyo Mkuu wa TFF, Kidao ameongeza ”Tunakubaliana TFF, Bodi ya Ligi, Kamati ya Waamuzi, Ninyi waandishi wa habari na Wadau mbalimbali kwamba kuna changamoto ya eneo hili.”

Siku za hivi karibuni kumekuwa na malalamiko kadhaa kutoka kwa wadau wa soka nchini yanayo lalamikia vitendo vya baadhi ya waamuzi kutosimamia sheri ipasavyo, hali iliyopelekea wengine kufungiwa na ahata kupata adhabu kali kutoka kwa Mamla zinazosimamia Mpira wa Miguu nchini.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents