Tupo Nawe

Waandamanaji Sudan wakaidi agizo hili la Jeshi, baada ya jeshi hilo kumpindua Bashir madarakani

Umati mkubwa umeendelea kuwepo katika mitaa ya mji mkuu wa Sudan , Khartoum, na kupuuza amri ya kutotoka nje wakati wa usiku iliyotangazwa na baraza jipya la jeshi nchini humo.

Kwa mujibu wa BBC. Kiongozi wa muda mrefu -Rais Omar al-Bashir alipinduliwa na kukamatwa siku ya Alhamisi baada ya miezi kadhaa ya maandamano.

Lakini waandamanaji wanasema baraza la jeshi ni sehemu ya utawala uliong’olewa madarakani. Kwenye mitandao ya kijamii kama huu wa Twitter, baadhi ya raia kama Alaa Salaa wameapa kuendelea kuandamana mpaka watakapopata uhuru kamili.

https://twitter.com/oalaa_salah/status/1116463540708286465/photo/1?ref_src=twsrc%5Etfw%7Ctwcamp%5Etweetembed%7Ctwterm%5E1116463540708286465&ref_url=https%3A%2F%2Fwww.bbc.com%2Fswahili%2Fhabari-47905430

View image on Twitter
View image on Twitter
View image on Twitter

Mwisho wa ujumbe wa Twitter wa @oalaa_sala

Hali mpya ya sintofahamu imeibua hofu kubwa ya uwezekano wa kutokea kwa makabiliano baina ya waandamanaji na jeshi.

Pia kuna hatari kubwa kwamba makundi tofauti ya usalama na wanamgambo wanaweza kupigana, anasema mhariri wa BBC Idhaa ya Dunia wa masuala ya Afrika Will Ross.

Umoja wa Mataifa na Muungano wa ulaya wametoa witoi wa kuwepo kwa hali ya utulivu.

Shamra shamra na sherehe zilizofuatia taarifa ya kukamatwa kwa Bwana Bashir mwenye umri wa miaka 75-zilikoma haraka pale waandalizi wa maandamano walipotoa wito wa wa watu kukaa nje ya makao makuu ya jeshi ili kuendelea na maandamano.

“Huu ni muendelezo wa utawala uliopo ,”alisema Sara Abdeljalil kutoka of Chama cha Wataalamu cha Sudan. “Kwa hiyo kile tunachokihitaji kukihfanya ni kuendelea kupambana na kupinga kwa amani.

Baadae, taarifa rasmi iliyotolewa na vyombo vya habari vya serikali vilisema kuwa tahadhali ya kutotoka nje itaanza kutekelezwa kuanzia saa nne za usiku majira ya Sudan

“Raia wanashauriwa kuizingatia kwa ajili ya usalama wao ,” ilisema taarifa hiyo na kuongeza kuwa: ” Wanajeshi na baraza la usalama wanatafanya kazi yao kuhakikisha inakuwepo hali ya amani na usalama na kuyalinda ”maisha ya raia .”

Waandamanji dhidi ya serikali wamekuwa wakiwaunga mkono wanajeshi
Image captionWaandamanji dhidi ya serikali wamekuwa wakiwaunga mkono wanajeshi

Umati wa watu kwenye mitaa ya mji wa Khartoum walipeperusha bendera na kushangilia “Uanguke, tena !” – wakirudia wito wao wa awali kumpinga Bashir uliosema “Aaangushwe , hicho ndio tunachokitaka !”.

Bwana Bashir anakambiliwa na kibali cha kukamtwa kilichotolewa na mahakama ya kimataifa ya uhalifu (ICC), ambayo inamshutumu kwa kupanga uhalifu wa kiviuta na uhalifu dhidi ya binadamu katika jimbo la magharibi mwa Sudan la Darfur.

Haijawa wazi ni kipi kitakachotokea kwake sasa kwani sasa yuko mahabusu.

Mapinduzi yalitokea vipi?

Mapema siku ya Alhamis , magari ya kijeshi yaliingia kwenye uwanja mkubwa wa majengo ya wizara ya ulinzi, ambako kuna makao makuu ya jeshi na makazi binafsi ya Bwana Bashir.

Televisheni na redio za taifa zikakatiza matangazo yake na waziri wa ulinzi Awad Ibn Ouf alitoa tangazo “la mapinduzi ya utawala “. alisema Bwana Bashir anashikiliwa “mahala salama” lakini hakutoa maelezo zaidi.

Omar al Bashir ni mmojawapo wa viongozi waliohudumu kwa muda mrefu duniani:

Omar al Bashir ni mmojawapo wa viongozi waliohudumu kwa muda mrefu duniani

Bwana Ibn Ouf alisema kuwa nchi imekuwa katika hali mbaya ya ” Utawala mbaya, ufisadi na ukosefu wa haki ya kisheria ” na akaomba msamaha “kwa mauaji na ghasia zilizotolkea “.

Alisema kuwa serikali itasimamia kipindi cha mpito cha miaka miwili kitakachofuatiwa na uchaguzi.

Waziri huyo pia alisema kuwa kipindi cha miezi mitatu cha dharura kimewekwa.

Utekelezwaji wa katiba ya Sudanumeahirishwa, na mipaka imefungwa hadi muda agizo jingine litakapotolewa na safari za anga zimeahirishwa kwa kipindi cha saa 24 ,aliongeza.

Hali tete isiyo ya kutabirika 

Haya ni mapinduzi ya kijeshi yasiyo na mwongozo wa wazi juu ya namana majenerali watakavyokabidhi madaraka kwa utawala wa kiraia.

Hofu itakuwa ni kwamba hawana nia ya aina hiyo . Wasomi wa usalama wamekwishaweka mipango kwamba kumuondoa Omar al-Bashir na kuweka tahadhari ya kutotoka nje vitawawezesha kuwa na muda na kusitisha maandamano. Kama hali ni hiyo haya yatakuwa ni makosa makubwa.

Chama cha wataalamu cha Sudan (SPA) – ambacho kimeongoza maandamano – na mashirika mengine ya kiraia wamekwisha kusema wazi kuwa kamwe hawatakubali mabadiliko bandia .Wana ufuasi mkubwa wa watu na wamejipanga ipasavyo.

Je mapinduzi ya kijeshi yanaongezeka Afrika?

Jeshi lina silaha na uwezo wa kufanya ukatili . Lakini itasaidia nini? kamata kamata haitaleta suluhu la mzozo wa kiuchumi wa muda mrefu ambao ndio uliowachochea raia kuingia mitaani mwezi wa Disemba.

Pia kuna tatizo la mpasuko ndani ya idara za usalama nchini Sudan ,ulioonekana wakati wa makabiliano baina ya wanajeshi na vikosi vya ujasusi katika siku za hivi karibuni.

Ni hali tete na ambayo haitabirikiinayojhitaji vichwa kutulia na muafaka upande upande wa jeshi. Uthabiti wa Sudani utategemea namna watakavyoshughulia matakwa ya waandamanaji.

Bwana Omar Al- Bashir

Chama cha wataalamu wa Sudani SPA kilisema kuwa jeshi lilitangaza”mapinduzi” na kwamba yataleta “surana na taasisi ambazo ni sawa sawa na zile ambazo watu wetu walizipinga”.

Kiliwataka watu kuendelea na mgomo wa kuketi nje ya majengo ya jeshi – ulioanza siku ya Jumamosi – na kukaa kwenye mitaa ya miji kote nchini.

“Wale walioharibu nchi na kuwauwa watu wanataka kuiba kila tone la damu na jasho ambalo sisi watu wa Sudan tulimwaga katika mapinduzi yaliyotikisa utawala dhalimu ,” ilisema taarifa yao iliyosomwa.

Awali SPA ilisema kuwa utawala wowote wa mpoto lazi ujumuishe yeyote kile walichokiita “utawala dhalimu”.

Namna maandamano yalivyoanza

maandamano yalianza mwezi Disemba. Mwanzo yalisababishwa na kupanda kwa gharama ya maisha, lakini baadae umati ukaanza kutoa wito kwa rais ajiuzuru na serikali yake iende.

Aliyekuwa rais wa Sudan Omar al-Bashir tarehe 12 Februari , 2019
Image captionOmar al-Bashir amekuwa madarakani tangu mwaka 1989

Maafisa wa serikali walisema kuwa watu 38 walikufa kufikia mwezi Disemba lakini shirika la haki za binadamu Human Rights Watch lilisema idadi ilikuwa ni ya juu zaidi.

Mwezi Februari ,ilionekana kana kwamba rais angejiuzuru , lakini badala yake Bwana Bashir alitangaza hali ya tahadhari ya taifa.

Jamii ya kimataifa inasema nini juu ya hali ya sasa nchini Sudan ?

Katibu Mkuu wa umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametoa wito wa kuwepo kwa hali ya “utulivu na ustahilimivu kwa wote” na akataka kuwepo kwa kipindi cha mpito kitakachotimiza ” matarajio ya demokrasia ” ya watu.

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa linatarajia kujadili hali ya mambo nchini Sudan katika kikao cha faragha Ijumaa.

Waziri wa mambo ya nje wa Uingereza Jeremy Hunt alisema kuwa baraza la kijeshi ”sio jibu”

“Tunahitaji kuona hatua haraka za kuleta utawala unaojumuisha na kuwakilisha uongozi wa kiraia . Na tunahitaji kuhakikisha kuwa hakuna ghasia ,” alisema kupitia mtandao wa Twitter.

Magufuli amtaka waziri ‘avute bangi’

Marekani imelitolea wito jeshi la Sudan kuwajumuisha raia katika serikali ya mpito na ikasema kipindi cha miaka miwili cha mpito ni kirefu sana.

Umoja wa Afrika umelaani mapinduzi ya kijeshi. Mwenyekiti watume ya Muungano huo Moussa Faki Mahamat alisema kuwa mapinduzi hayo hayakufaa kuwa jibu la changamoto zinazoikabili nchi na matarajio ya watu wake.

Urusi , ambayo ilimpokea mara mbili Bwana Bashir, ilitoa wito kwa hali ya utulivu na ikasema inafuatilia kwa karibu hali ya mambo nchini Sudan.

Katibu Mkuu wa Amnesty Internationa Kumi Naidoo amesema kuwa haki “ilicheleweshwa kwa muda mrefu ” kwa Bwana Bashir.

“Omar al-Bashir anatakiwa na mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC kwa ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu kuwahi kushuhudiwa katika kizazi hiki na tunahitaji hatimae kumuona akiwajibika ,” Aliongeza Bwana Naidoo.

Omar Omar al-Bashir ni nani?

Afisa wa zamani wa jeshi , alinyakua mamlaka katika mapinduzi ya kijeshi mnamo1989.

Utawala wake ulitawaliwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe . Mzozo wa kivita na Sudan Kusini ulimalizika mwaka 2005 na Sudan Kusini ikawa huru mwaka 2011.

Mzozo mwingine wa wenyewe kwa wenyewe umekuwa ukiendelea katika jimbo la magharibi mwa nchi hiyo la Darfur. Bwana Bashir anashutumiwa kwa kupanga uhalifu wa kivita na uhalifu wa kibinadamu katika mahakama ya ICC.

Licha ya kibali cha kukamatwa kutolewa na mahakamana ya ICC, alishinda mara mbili mfulurizo katika uchaguzi uliofanyika mwaka 2010 na ule wa 2015. Hata hivyo, ushindi wake wa mwisho ulisusiwa na vyama vikuu upinzani.

Kibali cha kumkamata kilisababisha kuwekewa marufuku ya kutosafiri katika mataifa ya kigeni. Hata hivyo Bwana Bashir alifanya ziara za kidiplomasia katika mataifa ya Misiri, Saudi Arabia na Afrika Kusini

Ramani inayoonyesha ilipo nchi ya Sudan

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW