Uncategorized

Waandamanaji Sudan washinikiza utawala wa kiraia

Wiki moja baada ya Omar al-Bashir kuondolewa madarakani maandamano katika mji mkuu wa Sudan, Khartoum yanaendelea kurindima.

Kwa mujibu wa shirika la habari la BBC, Waandamanaji hao wanasema kuwa hawataondoka barabarani hadi wapate mabadiliko ya kudumu.

Baraza la mpito linaloongozwa na jeshi limeahidi kuzingatia matakwa yao lakini waandamanaji wanahofia hatua waliopiga huenda ikahujumiwa ikiwa utawala utasalia mikononi mwa wanajeshi.T

Wamejikusanya katika eneo kubwa la katikati ya mji wa Khartoum karibu na makao makuu ya kijeshi, hali ambayo imesababisha msongamano mkubwa.

Hatua hiyo imevutia mashauriano ya ngazi ya juu huku wanasiasa na viongozi wa kijeshi wakilazimika kufanya kazi ya ziada kufikia utawala wa kiraia haraka iwezekanavyo.

Wachambuzi hata hivyo wanasema kujenga taifa litakalo heshimu utawala wa kidemokrasia baada ya kuwa chini ya utawala wa kijeshi kwa miaka 30 sio kitu ambacho kinaweza kufikiwa kwa muda wa wiki moja.

Waandamanaji Sudan
Image captionWaaandamanaji waameapa kutoondoka barabarani hadi wapate utawala wa kiraia

Wanasema Misri kwa mfano jeshi lina nguvu kubwa na hawako tayari kuachia madaraka kwasababu ya kuhofia hatma yao ya siku zijazo.

Chama cha wataalamu wasomi ambacho kimekua mstari wa mbele kuongoza maandamano hayo ni kiungo muhimu katika mazungumzo ya kubuniwa kwa serikali ya mpito ya kiraia.J

Makundi mengine kama yale ya kupigania Uhuru na Mabadiliko yamekuwa yakikutana na baraza la jeshi linaloongoza nchi kwa awamu ya mpito.

Makundi yote yanayoshinikiza kubuniwa kwa utawala wa kiraia yameungana ili kubuni muungano wa upinzani utakaosaidia kufikiwa kwa ndoto ya kupatikana kwa utawala wa kiraia Sudan.

Moja ya makundi hayo ni lile la Maprofesa kutoka Chuo Kikuu cha Khartoum.

Waandamanaji Sudan
Image captionMiezi kadhaa ya maandamano yalipelekea rais Bashir kung’olewa madarakani

Tangu wanafunzi wa vyuo vikuu walipoanza kuandamana mwezi Disemba mwaka Jana, mamia ya wasomi walijiunga nao kisiri-kwa kuwapatia mwongozo wa jinsi watakavyo endeleza juhudi ya kutaka mabdiliko.

“Watu walishangaa sana wakati maandamano haya yalipoanzishwa na wanafuzi. Tulifikiria hawana ufahamu kuhusu masuala ya kisiasa lakini tulikosea,” alisema profesa Intisar Soghayroun, mtaalamu wa masuala ya archaeolojia.

Maprofesa hao wamewashauri vijana kuendelea kuandamana hadi pale utawala wa mpito wa kijeshi utakapoitikia wito wao

“Mwanzoni hatukua na uhakika lakini sasa tumepiga hatua na ya kuwashawishi watu kutoka nje kwa wingi kuunga mkono juhudi hizi,” alisema.

Sudan protester
Image captionWaandamanaji na makundi ya upinzani wafanya mazungumzo na jeshi Sudan

Maelfu ya watu wamekua wakiandamana katika maeneo yaliyo karibu na makao makuu ya kijeshi wakupitia vizuizi vilivyowekwa na wapangaji wa maandamano hayo.

Lakini baadhi yao hawaamini ahadi iliyotolewa na baraza la kijeshi linaloongoza taifa hilo kwa awamu ya mpito ni za kutegemewa.

Watu wanataka kuona rais wa zamani wa taifa hilo Omar al-Bashir amefungwa na wale wote waliyotekeleza unyama chini ya utawala wake wachukuliwa hatua za kisheria

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents