Habari

Waandishi 6 wa Ivory Coast washtakiwa kwa kutoa taarifa za uongo

Waandishi na wahariri sita wa jarida moja la nchini Ivory Coast wameshtakiwa na serikali ya nchi hiyo kwa kueneza habari zisizokuwa na ukweli na kusababisha hofu ya usalama wa nchi.

Jarida hilo lilichapisha makala kuhusu uasi ambao ulifanywa wiki iliyopita na vikosi maalum vya nchi hiyo na kuripoti kuwa kwamba Wizara ya Ulinzi ya nchi hiyo imewalipa fedha nyingi wanajeshi hao ili kusitisha uasi huo na kurudi kazini.

Mwendesha mashtaka wa serikali wa nchi hiyo Adou Richard amesema, “Unfortunately we have noted that, in relation to these movements, certain media outlets are spreading false information that could incite soldiers to revolt.”

Waandishi hao walishikiliwa na polisi kwa siku mbili kuanzia Jumapili iliyopita na baadae wakaachiliwa huku kesi yao ikiendelea wakati huo huo kesi hiyo inaweza kuwasababishia hukumu ya kifungo cha mpaka miaka mitano.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents