Bongo Movie

Waandishi wazitambua mbinu za Lulu Mahakamani

Kesi ya kuuwa bila kukusudia inayomkabili muigizaji wa maigizo, Elizabeth Michael (Lulu) ikiendelea Mahakama Kuu ya Tanzania ikiwa ni siku ya sita mfululizo kuonekana Mahakamani hapo akiwa na style tofauti za uingia na utokaji ili kukwepa picha kwa waandishi.

Leo mapema wakati waandishi wa habari wakimsubiri msanii huyo, alikuja na style ya tofauti na ya ajabu kidogo buana, alicholifanya mtu wa kwanza wa karibu kuingia Mahakamani hapo alikuwa ni Munalove ambaye amekuwa akihudhuria kila siku katika kesi hiyo.

Mtu wa pili kufika pale alikuwa wakili wake Peter kibatala akiongozana na baba yake Lulu mwenyewe, huku ile gari iliyomshusha baba huyo, hata hivyo waandishi walikuwa wameikariri gari hiyo kwa kuwa mnara nyingi huja nayo Mahakamani hapo,basi naada ya ile gari kumshusha baba Lulu ikaenda mbele kwa spidi kama imeshawashusha wahusika na hakuna mwingine anayetakiwa kushuka. Waandishi hao waliokuwepo hapo hawakasema haiwezekani hawa wanatudanganya Lulu atakuwa yupo kwenye ile gari wakaenda kukaa mbele ya Mahakama ili wakijua kuwa ni lazima atapita mahakamani katika geti la mahahakamani hapo.

Baada ya dakika kadhaa Lulu alitokea Mbele ya Mahakama hiyo na mama yake, sehemu ambayo waandishi wa habari walifikiria lazima angekuwepo, hakuwa na namna akashuka akaingia Mahakamani hapo hakuwa na namna ya kuwakwepa waandishi hao na badala yake wakamuona na kupata picha na video mpaka ana kaa kwenye chumba cha Mahakama. Alipofika Mahakamani hapo alikuwa akificha sura ili waandishi wasipate picha.

Lulu anadaiwa kutenda kosa hilo Aprili 7,2012, nyumbani kwa Kanumba, Sinza Vatican jijini Dar es Salaam. Jaji Sam Rumanyika amesema hukumu itatolewa Novemba 13, mwaka huu.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents