Habari

Wabunge 29 wa Korea Kusini wajitoa chama tawala

Wabunge wapatao 29 wanaotoka kwenye chama tawala cha nchi hiyo wamejitoa kwenye chama hicho.

Sababu ya kujiondoa kwenye chama hicho imedaiwa kuwa ni kutokana na tuhuma nzito zinazomkabili Rais Park Geun-hye kutokana na sakata la rushwa pamoja na kutuimia madaraka yake vibaya.

Hata hivyo imeelezwa kuwa kuna uwezekano mkubwa kwa wabunge hao kuanzasha chama chao na kumfanya katibu mkuu wa umoja wa mataifa anayemaliza muda wake Ban Ki-Moon kuwa mgombea wao wa urais kwenye uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mapema mwakani.

Takribani miezi miwili sasa nchi ya Korea Kusini imekuwa katika hali mbaya ya kisiasa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents