Habari

Wabunge na madiwani wote wa Chadema wanakabiliwa na kesi mkoani Morogoro (+video)

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA), Freeman Mbowe amesema kuwa Wabunge wote wanne wanaotoka mkoa wa Morogoro wanakabiliwa na kesi, madiwani wote wa Chadema wanakabiliwa na kesi katika mkoa huo.

“Mkoa wa Morogoro unaongoza kwa kubambikiziwa kesi, Wabunge wote wanne wanaotoka mkoa wa Morogoro wanakabiliwa na kesi, madiwani wote wa Chadema wanakabiliwa na kesi katika mkoa wa Morogoro, madiwani watatu mpaka leo wamefungwa jela kwa makosa ya kubambikiziwa ya kisiasa na tunavyozungumza hivi viongozi wetu 40 wa morogoro mjini wanahudhuria kesi ya kisiasa iliyotokana na uchaguzi mdogo wa Kata ya Sofi ambapo Chadema ilishinda ambapo NEC kwa kushirikiana na serikali ikaamua kubadilisha matokeo,” alisema Mbowe.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents