Habari

Wabunge upinzani wasusia kiapo cha wabunge wateule CUF

Wabunge wa kambi rasmi ya upinzani bungeni wamegomea shughuli za kiapo cha wabunge wateule wa Chama cha wananchi (CUF) ili kuwaunga mkono wabunge waliovuliwa uanachama na kupoteza ubunge pamoja na kupinga bunge kutumika na serikali kukandamizi upinzani.

Wabunge wa upinzani wakiwa nje ya Bunge wakati wabunge wapya wa CUF wakiapishwa Bungeni leo asubuhi.

Wakizungumza katika viwanja vya Bunge, huku wabunge wateule wakiendelea kuapishwa ndani ya Bunge, Katibu wa Kambi rasmi ya upinzani bungeni Mhe David Silende amesema kambi rasmi ya upinzani haitawapa ushirikiano wabunge hao mpaka kesi ya msingi itakapo malizika mahakamani.

Kwa upande wake Katibu wa Bunge wa Chama cha wananchi (CUF), Bwana Juma Kombo Hamad amesema vyama vya upinzania vinadai haki itendeke katika masuala yote ya msingi na kusisitiza kinacholalamikiwa ni kufukuzwa kwa wabunge katika chama ambacho kina mgogoro haukufuata misingi ya sheria na Katiba.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents