Michezo

Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muuungano wa Tanzania, wamehamasika kuichagia timu ya Serengeti Boys

Wakati timu ya Taifa ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 ya Tanzania maarufu kama Serengeti Boys ikirejea salama jijini Dar es Salaam salama ikitokea Dodoma, Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muuungano wa Tanzania, wamehamasika kuchagia timu hiyo.

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Job Ndugai alikuwa mstari wa mbele kutoa hamasa hiyo wakati wa matangazo mbalimbali mara baada ya kipindi cha maswali na majibu katika kikao cha bunge.

Wazo lilitoka kwa Mbunge wa Bunda, Mheshimiwa Esther Bulaya aliyetaka mwongozo wa Mheshimiwa Spika kwa timu ya Serengeti Boys kufanya vema katika michuano ya kufuzu kwa fainali za Vijana ambazo zitafanyika kuanzia Mei 21, mwaka huu huko Gabon.

Alisimama kutoa mwongozo huo huku akipendekeza kwa Wabunge wenzake wakubali kukatwa angalau posho ya siku moja kuchangia timu hiyo ambayo bajeti inaonesha kwamba maandalizi yake na kiushiriki michuano hiyo kunahitajika zaidi ya Sh bilioni moja.

Wabunge waliopewa nafasi ya kuchangia hoja hiyo walikubali kuchangia kwa sababu mfumo huo unafanywa pia na mataifa mengine na waliwatia shime vijana hao kwenda kupambana Gabon na kurejea nyumbani Tanzania na kikombe cha Afrika wakiwa ni mabingwa wa vijana wenye umri wa chini ya miaka 17.

Awali, vijana hao kabla ya kuingia ukumbini walikutana na Bibi yao, Mheshimiwa Margaret Sitta – Mbunge wa Urambo na kuwazawadia fedha Sh 100,000 aliyeonesha furaha yake kwa vijana hao kufanya vema awali kabla ya kufuzu kucheza fainali kabla ya vijana hao kumshukuru Mama Sitta.

Baadaye, Mheshimiwa Mbunge Almas Maige aliwatuza Sh 500,000 na Mheshimiwa Bulaya akatoa Sh 300,000 hivyo kufanya jumla ya fedha hiyo kuwa Sh 900,000 ambazo Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi kuamuru kupewa vijana hao.

Rais Malinzi aliyeongoza msafara huo bungeni, alitoa shukrani nyingi kwa Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mheshimiwa Nape Nnauye kwa kuwaalika Serengeti Boys bungeni.

Alishukuru kwa jinsi wabunge walivyojitoa kuahidi kuchagia gharama za maandalizi na kushiriki kwa timu hiyo katika michuano hiyo mikubwa ya soka kwa vijana ambayo fainali zake zitachezwa Juni 4, mwaka huu.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents