Siasa

Wabunge wa Malawi wakataa msaada wa kondomu, Hatutaki tuna uwezo wa kujinunulia wenyewe

Wabunge nchini Malawi wamekataa kupokea msaada wa mipira ya kondomu zaidi ya 200,000 waliyopewa na shirika moja la kutoa misaada.

Mipira hiyo ilikuwa iwekwe katika vyoo vya majengo ya bunge.

Kiongozi wa wengi bungeni, Richard Chimwendo, amesema wabunge hawahitaji msaada huo kwasababu wana uwezo wa kujinunuliwa mipira ya kondomu.

Msaada huo ulipewa mwenyekiti wa kamati ya, Maggie Chinsinga.

Bw. Chimwendo alisema ripoti iliyochapishwa na gazeti moja nchini humo kwamba msaada huo umewadhalilisha wabunge.

Ripoti hiyo ilimnukuu Bi Chinsinga akisema kuwa bunge hutumia karibu mipira 10,00 ya kondomu kila mwezi na kwamba wakati mwingine “zinaisha”, iliandika gazeti laNation nchini Malawa.

Naibu wa Spika, Madaliotso Kazombo, amekanusha madai haya na kutaka gazeti hilo kuomba radhi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents