Habari

Wabunge wa Ukawa waendelea kususia vikao vya Bunge

Wabunge wanaoiunda umoja wa katiba ya wananchi (UKAWA) wameendelea kutoka nje ya Bunge ikiwa ni siku ya mwisho ya kupitisha bajeti ya serikali kwa mwaka wa fedha 2016-2017.

B80vBQxcuTO8QAAAABJRU5ErkJggg==

Wabunge hao wametoka nje ya Bunge hilo wakiwa wameziba midomo kwa kutumia karatasi na plasta huku wabunge wa chama tawala wakiendelea na kazi yao kama kawaida na maswali ambayo walilenga kuuliza wabunge wa upinzani yakiulizwa na wabunge wa chama tawala kwa niaba yao.

Nje ya ukumbi wa Bunge, wabunge hao wamesema wamefanya hivyo kuonyesha kwamba Bunge limekataa kusikiliza hoja zao za msingi walizoziwasilisha hapo awali.

Akizungumza kwa niaba ya wenzake, Mbunge wa Jimbo la Vunjo, James Mbatia amesema kwamba hawatakubali nchi hii iongozwe kwa fikra za mtu mmoja pia wanasikitishwa na kitendo cha wabunge wa chama tawala kuwatukana huku Naibu Spika akikaa kimnya.

“Hii ni ishara ya kuonyesha kwamba hasira zetu hatutakubali wakituzima midomo bungeni nje hawatatuzima juzi tumesusia hadi futari kuonesha kwamba hatukubaliani nao,” alisema Mbatia.

Aidha kwa muda wa wiki tatu mfulilizo wabunge wa upinzani wameendelea kususia vikao vya Bunge kwa madai ya kupinga Bunge hilo kuongozwa na Naibu Spika, Tulia Ackson.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents