Wabunge walipania Bunge la 12

Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania linatarajiwa kuanza mkutano wake wa 12 kesholitakalojadili bajeti ya mwaka ujao wa fedha, imegundulika kuwa wabunge kadhaa wamepania kutaka maelezo zaidi kuhusu mapesa yaliyochotwa Benki Kuu,

Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania linatarajiwa kuanza mkutano wake wa 12 kesholitakalojadili bajeti ya mwaka ujao wa fedha, imegundulika kuwa wabunge kadhaa wamepania kutaka maelezo zaidi kuhusu mapesa yaliyochotwa Benki Kuu, BoT kupitia akaunti ya madeni ya nje, EPA na hivyo kulifanya litarajiwe kuwa ni la aina yake.

Mpaka sasa baadhi ya wabunge wamesema wataibana Serikali ili ieleze hatua iliyofikiwa katika kufuatilia mapesa hayo, zaidi ya Sh.Bilioni 133 na kisha ifafanue ni kwa namna gani pesa hizo zimeingizwa katika matumizi ya bajeti ya mwaka ujao wa fedha.

Mbunge wa Jimbo la Karatu (CHADEMA), Dk. Wilbroad Slaa, amedai kuwa kamwe hatakubali kunyamazia suala hilo la mapesa ya EPA pasi na kupata maelezo ni kwa namna gani wananchi watanufaika kupitia bajeti watakayoijadili.

“nitahakikisha naendeleakuibana serikali mpaka nitakapopata majibu ya kueleweka kuhusiana na fedha hizo za zilizobainika baada ya uchunguzi uliofanyika” alisema Dk Slaa.

Akasema Dk. Slaa kuwa fedha hizo ni za wananchi na hivyo ni lazima wapate majibu kwa kile walichokuwa wakikitarajia baada ya kuambiwa kuwa kuna baadhi ya fedha hizo zimeanza kurejeshwa.

“Ni matarajio ya wananchi kuona fedha zilizorudishwa zinawasaidiaje katika bajeti ijayo… na mimi na wabunge wenzangu , kazi yetu ni kuikumbusha Serikali kuhusu fedha hizo” -Dkt. Slaa.

Kuhusiana na hoja binafsi, Dk. Slaa amesema huenda zisiwepo kwakuwa kanuni za Bunge la bajeti, zinataka kuzungumziwa kwa bajeti zaidi, licha ya kwamba zinaweza kuibuka endapo kutakuwa na umuhimu wa kufanya hivyo.

 

 

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents